Mauritius wachagua wabunge leo


Mauritius
Mauritius leo inafanya uchaguzi wa wabunge, huku vyama vilivyoungana vikipambana kupata asilimia kubwa ya viti.
Muungano wa kwanza wa Vyama vilivyoungana ni ule wa Chama cha Labour kikiongozwa na Waziri Mkuu Navinchandra Ramgoolam na cha Militant Movement ama MMM ambao wanataka mabadiliko ya katiba iwapo watashinda.
Muungano wa pili ni ule unaovileta pamoja vyama vya Militant Socialist Movement na kile cha Mauricien Social Democrate.
Uchaguzi wa bunge unaofanyika leo, unafuatia kampeni zilizokuwa zimetawaliwa na wanasiasa waliokuwa wakiahidi kufufua uchumi, na kutatua tatizo la ajira.
Uchaguzi huo ni muhimu kwa uchumi wa nchi hiyo.

                  via BBC

0 maoni:

Post a Comment