Hillary Clinton atangaza kugombea uraisiii
Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani, Bi Hillary Clinton ametangaza rasmi kuingia katika kinyang'anyiro cha urais wa nchi hiyo katika uchaguzi wa 2016 ambapo anataka kuwa mwanamke wa kwanza kuwa rais wa Marekani.
Alizindua ukurasa wake wa kampeni katika mtandao wa internet, Jumapili, akiwaambia Wamarekani kuwa anataka kuwa "kiongozi" wao.
Bibi Clinton aliingia katika mbio za kuomba kuteuliwa na chama cha Democratic kuwa mgombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2008 lakini alishindwa kwa Bwana Barack Obama.
Akiwa mgombea anayepewa nafasi na wanachama wa Democratic alitarajiwa kutangaza azma yake ya kugombea miezi kadhaa iliyopita.
Katika video kupitia ukurasa wake wa kampeni, Bibi Clinton alitangaza: "Nagombea urais".
"Wamarekani wamepambana na nyakati ngumu za uchumi," amesema, "lakini hali imebaki kuwanufaisha walio juu.
"Kila siku Wamarekani wanataka kiongozi na nataka kuwa kiongozi," amesema
Bibi Clinton pia alikuwa mke wa rais wakati mumewe Bill Clinton alipokuwa rais wa Marekani.
0 maoni:
Post a Comment