Ziara hiyo ya simba SC katika kituo hicho ni kwa ajili ya kumuenzi marehemu Sylveser Marsh aliyeifanyia mambo makubwa soka la Tanzania.
Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema wanakwenda kwenye kituo hicho kuonyesha wanamuenzi Marsh lakini kuonyesha Simba inajali ukuzwaji wa wachezaji vijana.
"Kuhusiana na vijana, Simba ni timu inayojali vijana na ndiyo timu inaongoza kutumia vijana hata katika kikosi chake kikubwa.
"Hivyo tutafika pale kutembelea kituo hicho, tutatoa rambirambi na kumuenzi Marsh ambaye alitoa mchango mkubwa kwa vijana wakati wa uhai wake," alisema Manara.
Baada ya ziara hiyo hapo kesho Simba SC siku ya jumamosi wanataaji kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Toto Afrika, ikiwa ni sehemu ya kuwakaribisha Toto Afrik katika ligi kuu ya vodacom.
Manara alisema kuwa Simba juma mosi watawakribisha Toto Afrika katika ligi ku ya vodacom kabla ya jumapili kuanza safari ya kurejea Dar es salaam na jumatano kuanza safari yakwenda Mbeya kuwakabili Mbeya city katika uwanja wa Sokoine.
Simba SC wapo Mwanza baada ya kumaliza mchezo wao dhidi ya Kagera sugar uliochezwa katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga siku ya jumatatu ya wiki hii.
0 maoni:
Post a Comment