BIBI AMCHOMA VISU VYA MOTO MJUKUU WAKE KISA KAPOTEZA PENI (Kalamu) YA SHILINGI 200.
Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza linamshikilia bibi mmoja aitwaye Laurencia Athanas mkazi wa Kiseke, Ilemela jijini Mwanza kwa tuhuma za kumchoma visu vya moto mjukuu wake na kumsababishia majereha mbalimbali mwilini akimtuhumu kupoteza peni (kalamu) ya shilingi 200.
Mtoto huyo aitwaye Jackson Hosea ( 10 ) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Kiseke iliyoko Ilemela Jijini Mwanza alifanyiwa unyama huo nyumbani kwa bibi huyo ambaye ni mzazi wa mama yake aishiye Nzega siku ya Ijumaa jioni tarehe 23 Mei 2015.
0 maoni:
Post a Comment