AZAM KUMNYEMELEA MCHEZAJI WA MBEYA CITY ,MAHUNDI

NA YOHANA EMMANUEL

Katika kuhakikisha inaboresha kikosi chake katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili, klabu ya Azam FC ipo kwenye mazungumzo na mchezaji wa Mbeya City Joseph Mahundi  kwa ajili ya kukamilisha deal la usajili.

Afrsa habari wa Azam FC Jafar Idd aliiambia Clouds FM kuwa, Azam wapo kwenye mazungumzo ya mwisho na Mhundi na kama kila kitu kitakwenda sawa basi atavaa uzi wa klabu yao kuanzia raundi ya pili ya msimu huu wa ligi kuu Tanzania bara.
“Tunamazungumzo na mchezaji Joseph Mahundi ambaye anacheza Mbeya City, kama tutakubaliana na mchezaji huyu tutawaambia, Jafar Idd amenukuliwa na kipindi cha Sports Extra cha Clouds FM.
“Mwalimu mwneyewe Zeben Hernandez alimuona akasema anamuhitaji kwenye kikosi chake, kama mazungumzo yakienda vizuri basi atakuwa mchezaji pekee wa kitanzania kusajiliwa Azam katika msimu huu.”
Jafar Idd pia amesema tayari wameshaituma ITC ya beki wao wa zamani Pascal Wawa kwenda kwenye klabu ya Al Mereikh ya Sudan aliyojiunga nayo baada ya mkataba wake na Azam kumalizika hivi karibuni.

0 maoni:

Post a Comment