Mufti Issa Shaaban bin Simba enzi za uhai wake
|
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ameongoza maelfu ya waumini wa dini ya kiislamu na watu mbalimbali wenye mapenzi mema kumzika Shehe mkuu wa Tanzania Mufti Issa Shaban Simba katika makaburi ya waislam ya Nguzo nane mjini Shinyanga.
Mazishi hayo yamefanyika leo jioni na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini ya kiislamu,wakristo na viongozi wa serikali ,wanasiasa ambao walijitokeza kumzika Mufti Simba aliyefariki dunia jana akipatiwa matibabu kutokana na kusumbuliwa sana na sukari,Shinikizo la Damu (BP) pamoja na Figo.
Katika mazishi hayo,mawaziri wakuu wastaafu Mheshimiwa Edward Lowassa na Fredrick Sumaye walikuwepo,viongozi wengine ni mheshimiwa Lazaro Nyalandu,Benard Membe,William Ngeleja,Patrobas Katambi,Stephen Masele,askofu Liberatus Sangu n.k
Mwili wa marehemu uliwasili mchana mjini Shinyanga ukitokea jijini Dar es salaam na kufikishwa nyumbani kwa marehemu katika mtaa wa Majengo kata ya Kambarage katika manispaa ya Shinyanga.
Baadaye mwili ulipelekwa katika msikiti wa Masjidu Thaqafal Abdallah Islamiya uliopo Majengo mjini Shinyanga kwa ajili ya sala ya alasiri/kuombewa dua kisha mwili huo kupelekwa katika makaburi ya waislamu ya Nguzo Nane kwa ajili ya Mazishi.
Mufti Simba alizaliwa mwaka 1939,ameacha mjane na watoto 11.
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,ndugu Kadama Malunde alikuwepo eneo la tukio ametuletea picha zaidi ya 60 angalia hapa chini
|
|
Nyumbani kwa marehemu- MTAA WA MAJENGO MJINI SHINYANGA-Ndugu wa marehemu wakijiandaa kupkea mwili wa marehemu ukitoka jijini Dar es saalam |
|
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Mussa Salum akiongea jambo na meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam nyumbani kwa marehemu mtaa wa Majengo mjini Shiyanga |
Shehe wa wilaya ya Shinyanga akitoa maelekezo msibani
|
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu |
|
Viongozi mbalimbali wa dini ya kiislam nchini wakiwa msibani |
|
Waombolezaji wakiwa msibani |
|
Waombolezaji wakiwa msibani |
|
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Mussa Salum akiongea jambo na waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa nyumbani kwa marehemu |
|
Mbunge wa jimbo la Solwa Ahmed Salum akiwa na mheshimiwa Lowassa |
|
Mawaziri wastaafu Edward Lowassa na Fredrick Sumaye wakisalimiana msibani |
|
Maelfu ya waombolezaji wakiwa msibani |
|
Jeneza lililobeba mwili wa Mufti Alhaj Sheikh Shaaban bin Simba kuelekea katika msikiti wa wa Masjidu Thaqafal Abdallah Islamiya uliopo Majengo mjini Shinyanga kwa ajili ya sala ya alasiri |
|
Mwili wa marehemu ukiwa kwenye jeneza |
|
Mwili wa marehemu ukipelekwa msikitini |
|
Mwili wa marehemu ukipelekwa msikitini |
|
Waombolezaji wakiwa wamejipanga barabarani |
Mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi akitoa maelekezo kwa waombolezaji waliokuwa barabarani
Baadhi ya waombolezaji wakiwa nje ya msikiti
Mwili wa marehemu ukiingizwa msikitini kwa ajili dua ya kumuombea marehemu.Msikiti huo wa Ijumaa wa Majengo mjini Shinyanga ni ule ambao kabla Mufti Issa Bin Shaban Simba alikuwa shehe wa msikiti huo
|
Akina mama hawakuwa nyuma,wakaamua kujipanga barabarani |
Waombolezaji wakiwa barabarani kusubiri mwili wa marehemu utolewe msikitini na kuupeleka makaburini
Sheikh wa mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya(kulia) akiwa katika makaburi ya Nguzo nane mjini Shinyanga
|
Waombolezaji wakiwa katika makaburi ya Nguzo nane mjini Shinyanga |
|
Wakazi wa Shinyanga wakiwemo wakuu wa wilaya za Kahama na Kishapu wakiwa katika makaburi ya Nguzo nane |
|
Viongozi mbalimbali wakiwa katika makaburi ya Nguzo nane |
|
Viongozi mbalimbali wakiwa makaburini |
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja(kulia) akiwa nje ya geti la makaburi ya Nguzo nane
|
Waombolezaji wakigombania kuingia makaburini |
Rais Kikwete akiwa katika makaburi ya Nguzo nane,wa kwanza kushoto ni kadhi mkuu wa Tanzania Sheikh Mnyasi,akifuatiwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga
Waombolezaji wakiwa katika makaburi ya Nguzo nane
|
Shughuli za Mazishi zinaendelea |
|
Waombolezaji wakiwa makaburini |
|
Rais Kikwete akiwa ameshika tama makaburini |
|
Mdogo wake na marehemu Ramadhani Simba akiweka udongo kaburini |
|
Rais Kikwete akiweka udongo kaburini |
|
Kadhi mkuu wa Tanzania Sheikh Yusuph Bin Abdallah Mnyasi akiweka udongo kaburini |
|
Mheshimiwa Fredrick Sumaye akiweka udongo kaburini |
Mheshimiwa Edward Lowassa akiweka udongo kaburini
Mheshimiwa Khamis Mgeja akiweka udongo kaburini
|
Mheshimiwa Bernard Membe akiweka udongo kaburini |
|
Rais Kikwete akiwa katika makaburi ya Nguzo nane |
|
Mazishi yanaendelea |
Waombolezaji wakiwa eneo la tukio
|
Kaburi la Mufti Alhaj Sheikh Shaaban bin Simba katika makaburi ya Nguzo nane mjini Shinyanga. |
|
Dua inaendelea |
|
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimpokea mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete nyumbani kwa marehemu katika mtaa wa Majengo mjini Shinyanga kwa ajili ya kuwapa mkono wa pole ndugu na jamaa wa marehemu |
|
Rais Kikwete akishikana mkono na sheikh wa mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya |
|
Rais Kikwete akishikana mkono ana askofu wa kanisa katoliki Jimbo la Shinyanga Liberatus Sangu |
|
Rais Kikwete akiwa nyumbani kwa marehemu |
|
Rais Kiwete akiwapungia mkono waombolezaji akiondoka mjini Shinyanga |
|
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu |
|
Mheshimiwa Lazaro Nyalandu akizungumza nyumbani kwa marehemu baada ya mazishi |
|
Mheshimiwa Lazaro Nyalandu akizungumza nyumbani kwa marehemu baada ya mazishi,nyuma yake ni mwenyekiti wa baraza la vijana Chadema taifa,Patrobas Katambi.
Mheshimiwa William Ngeleja akiwa nyumbani kwa marehemu akitoa mkono wa pole kwa ndugu jamaa na marafiki
Mheshimiwa Ngeleja akitoa mkono wa pole kwa mtu mmoja baada ya mwingine
Mheshimiwa Ngeleja akiwa msibani
Mheshimiwa Ngeleja akiondoka msibani.
Marehemu alijiunga na BAKWATA mwaka 1968 na amekuwa mwalimu wa chuo katika mikoa mbalimbali ya Mwanza, Bukoba na Mwaka 1970 alikuwa Shekhe wa Mkoa wa Shinyanga.
|
0 maoni:
Post a Comment