MWIGULU NCHEMBA AJIUZULU WADHIFA WAKE WA UNAIBU KATIBU MKUU WA CCM TANZANIA BARA
----
Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM -Bara,Mwigulu Nchemba amejiuzulu wadhifa huo.
Mwigulu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha,ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo Jioni katika kikao cha Halmashauri Kuu ya ya Taifa ya CCM,Mjini Dodoma
Akithibitha tukio hilo,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi ,Nape Nnauye amesema,Mwigulu ameamua kujiuzulu nafasi ya Unaibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara kutokana na nia yake ya kutaka kuomba kuwania Urais kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi utakaofanyika Octoba Mwaka huu
Mwigulu alishakuwa amemwambia nia hiyo Mwenyekiti wa Chama Rais Jakaya Kikwete,nae Rais akamkubalia, na sasa leo katika kikao ameomba rasmi kujiuzulu na Mwenyekiti Rais Jakaya Kikwete amemkubalia Mbele ya wajumbe wa NEC hii leo'..amesema Nape
Nape amesema kufwatia uamuzi wa mwigulu Mwenyekiti wa Chama Rais Jakaya Kikwete katika nafasi yake amemteua Msaidizi wake maswala ya siasa,Rajabu Ruhavi kuwa Mjumbe wa NEC na Wakati huohuo kumteua kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM -Bara Kushika nafasi iliyoachwa na Mwigulu Nchemba
0 maoni:
Post a Comment