Wanafunzi wanaosoma katika chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi
Shinyanga (Moshi Cooperative University-MOCU) wakiongozwa na rais wao
Bright Dominic Muro leo wametembelea kituo cha Kulelea watoto wenye
ulemavu
wa ngozi(albino),wasiosikia na wasioona cha Buhangija Katika manispaa ya
Shinyanga.
Wakiwa katika kituo hicho wametoa misaada mbalimbali ikiwemo unga wa
sembe
kilo 100,maharage kilo 100,unga wa lishe kilo 40,sabuni ,madaftari
makubwa,mafuta ya kupikia na yale ya kujipaka,kalamu,nguo na viatu vyote
vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi 500,000/=.
Wanafunzi hao pia wameshiriki shughuli mbalimbali ikiwemo kufanya usafi wa
mazingira na kufua nguo za watoto wanaolelewa katika kituo hicho cha Buhangija
ambacho sasa kinalea watoto zaidi ya 400 wengi wakiwa ni wenye ulemavu wa
ngozi wakikabiliwa na changamoto kubwa ya chakula.
|
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wajiandaa kuchoma moto taka zilizopo katika kituo cha Buhangija mjini Shinyanga |
|
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wakifanya usafi katika kituo cha Buhangija,kushoto ni mwalimu mlezi wa watoto wenye ulemavu katika kituo hicho |
|
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wakiendelea kufanya usafi |
|
Katibu wa kamati ya mfuko wa uchangiaji kwa ajili watu wenye ulemavu wa ngozi kutoka chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga Emmanuel Patrick akiwa amebeba uchafu katika kituo cha Buhangija |
|
Katibu wa kamati ya mfuko wa uchangiaji kwa ajili watu wenye ulemavu wa ngozi kutoka chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga Emmanuel Patrick akizubua mtaro wa maji machafu |
|
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wakichoma moto taka,kushoto ni mwenyekiti wa kamati ya mfuko wa kuchangia
albino katika chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga
(MOCU) Neema Medard Ngaita |
|
Wanafunzi hao wakifua nguo za watoto wa kituo cha Buhangija,katikati ni
mwenyekiti wa kamati ya mfuko wa kuchangia albino katika chuo kikuu cha
Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga (MOCU) Neema Medard Ngaita |
|
Zoezi la kufua nguo linaendelea-Aliyesimama ni Rais wa serikali ya Wanafunzi wanaosoma katika chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga (MOCU) Bright Dominic Muro |
|
Mwanafunzi wa MOCU Rehema Yateri akiwa amebeba ndoo ya maji na beseni kwa ajili ya kufua nguo za watoto hao |
|
Wanafunzi wanaosoma katika chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi
Shinyanga (MOCU) wakiendelea na zoezi la kufua nguo |
|
Mwalimu wa elimu Maalumu katika shule ya msingi Buhangija Sasu Nyanga
akizungumza kwa niaba ya mkuu wa kituo cha Buhangija ambapo mbali na
kuwashukuru wanafunzi hao kwa kujitolea kuwasaidia watoto hao , aliitaka
jamii
kuendelea kuwasaidia watoto wanaolelewa kituoni hapo ambao sasa wako zaidi
ya 400.
|
Wanafunzi wanaosoma katika chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga (Moshi Cooperative University-MOCU) wakiwa katika kituo cha Buhangija kabla ya kukabidhi msaada wao
|
Mwalimu wa elimu Maalumu katika shule ya msingi Buhangija Sasu Nyanga
alisema hivi sasa kutokana na ongezeko la watoto katika kituo hicho kuna
changamoto ya chakula ambapo mlo mmoja tu wa watoto hao ni Kilo 45 za
maharage,kilo 75-80 za mchele na unga kilo 70.
Wanafunzi wanaosoma katika chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga (Moshi Cooperative University-MOCU) wakiwa na watoto katika kituo cha Buhangija
|
|
Mwalimu wa elimu Maalumu katika shule ya msingi Buhangija Sasu Nyanga alisisitiza umuhimu wa wadau mbalimbali kuendelea kufika katika kituo hico kuwasaidia watoto hao |
|
Rais wa serikali ya Wanafunzi wanaosoma katika chuo kikuu cha Ushirika Moshi
tawi la Kizumbi Shinyanga (MOCU) Bright Dominic Muro akizungumza wakati
wa kukabidhi msaada wa chakula na mahitaji mengine muhimu,ambapo aliitaka
jamii kushirikiana na serikali katika kupiga vita mauaji ya watu wenye ulemavu
wa ngozi nchini Tanzania |
|
Rais Muro alisema amani ya taifa siyo tu taifa kuwa huru dhidi ya vita wala mapigano bali ni watu wanaoishi katika taifa hilo kuwa na amani hivyo kuitaka jamii kwa kushirikiana na serikali kupiga vita kwa nguvu zote mauaji ya abino yanayowafanya waishi bila amani katika taifa lao. |
|
Kulia ni rais wa serikali ya Wanafunzi wanaosoma katika chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga (MOCU) Bright Dominic Muro akikabidhi boksi la madaftari kwa Mwalimu wa elimu Maalumu katika shule ya msingi Buhangija Sasu Nyanga kwa niaba ya mkuu wa kituo cha Buhangija |
|
Rais wa serikali ya Wanafunzi wanaosoma katika chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga (MOCU) Bright Dominic Muro na Katibu wa kamati ya mfuko wa uchangiaji kwa ajili watu wenye ulemavu wa ngozi kutoka chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga Emmanuel Patrick wakikabidhi gunia la maharage |
|
Katibu wa kamati ya mfuko wa uchangiaji kwa ajili watu wenye ulemavu wa ngozi kutoka chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga Emmanuel Patrick akikabidhi mafuta ya kujipaka na kalamu kwa ajili ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija |
|
Rais wa serikali ya Wanafunzi wanaosoma katika chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga (MOCU) Bright Dominic Muro na Katibu wa kamati ya mfuko wa uchangiaji kwa ajili watu wenye ulemavu wa ngozi kutoka chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga Emmanuel Patrick wakikabidhi mafuta ya kupikia |
|
Tunafuatilia kinachoendelea....... |
|
Baada ya zoezi la kukabidhi misaada kumalizika-Wasanii kutoka MUCO Michael Onesmo na Gabriel wakiimba nyimbo maalum kwa watoto hao |
|
Zoezi la kupiga picha za kumbukumbu likaendelea |
|
Picha ya kumbukumbu |
0 maoni:
Post a Comment