BURUNDI YAAHIRISHA UCHAGUZI WA WABUNGE



Serikali ya Burundi imetangaza kuwa uchaguzi wa rais na wabunge uliotarajiwa kufanyika Ijumaa hii umehairishwa mpaka tarehe nyingine itakapopangwa.
Msemaji wa rais Nkurunzinza,Wily Nyamitwe ameiambia BBC kuwa tarehe itapangwa na wasimamizi wa uchaguzi wa nchi hiyo.


Mabadiliko hayo yamekuja kutokana na taifa hilo kuingia kwenye machafuko tangu Rais Piere Nkurunzinza kutangaza nia ya kuongoza kwa awamu ya tatu baada ya kuwa rais kwa miaka 10.
Umoja wa Mataifa imeelezea jinsi mgogoro huo ulivyoongeza idadi ya wakimbizi wanaoikimbia Burundi.
Hivyo kumtaka rais huyo kuachia ngazi mwezi huu kama makubaliano ya Azimio la Arusha yalivyoelekeza.

0 maoni:

Post a Comment