Edson Kamukara enzi za uhai wake |
Taarifa zilizokifikia chumba cha habari zinaarifu kuwa Mwandishi wa habari Edson Kamukara aliyewahi kuandikia gazeti la Tanzania Daima na baadae kuhamia Mwanahalisi, amefikwa na umauti leo jioni baada ya kulipukiwa na jiko la gesi nyumbani kwake Mabibo jijini Dar es Salaam.
Aidha habari kutoka kwa majirani zinaarifu kuwa Kamukara amerejea kutoka Bukoba, na alijisikia vibaya wakati anaenda dukani kununua dawa akaanguka na majirani kusaidia kumpepea na baade kupelekwa kwake ambako alipumzika hadi alipopata nguvu na kuamua kujiandalia chakula na ndipo ajali hiyo kumfika na kugharimu maisha yake.
Mwandishi nguli wa habari,Dotto Bulendu,katika ukurasa wake wa Facebook ameandika haya:
NAKULILIA EDSON KAMUKARA
Ulinikuta Chuo Kikuu nikiwa mwaka wa tatu,ghafla ukawa rafiki yangu wa karibu,ulipenda sana vipindi vyangu nilivyokuwa naendesha pale kwenye kituo cha redio cha chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino(Mwanza)(RADIO SAUT),nikiwa mwanafunzi nilikuwa naendesha kipindi cha majadiliano kinachoitwa MTAZAMO MKALI,uliniomba kuja kutazama navyokifanya.
Ulikuja kama mtazamaji mara tatu,baadae nikakuachia uwe unakiendesha,ukawa mahiri sana,nilipomaliza Chuo,niliajiriwa hapo Chuo Kikuu kama mkurugenzi wa kituo cha redio cha chuo kikuu,ili kuifanya redio ishindane,niliimua kutengeneza timu ya kunisaidia,EDSON KAMUKARA ulikuwa chaguo langu.
Nikakuomba ukubali kuwa meneja wa vipindi na kuwa msaidizi wangu mkuu,ulifanya kazi hiyo mpaka ulipomaliza masomo yako ya Chuo Kikuu,ulijiunga na gazeti la majira.
Kabla hujaacha kazi gazeti la majira na kwenda Jambo leo,uliniomba ushauri,na hata ulipoamua kuondoka Jambo leo uliniomba ushauri,nakumbuka wakati unaondoka gazeti la Jambo leo,ulinipigia simu saa sita usiku na kuniambia,"Brother naondoka jambo leo".
Ukanieleza kinagaubaga sababu za kuacha kazi Jambo leo,nami nikakuambia tafuta maisha zaidi ya hayo,ukaondoka na kwenda Tanzania Daima.
Kuwepo kwako Tanzania Daima,kulinifanya nami kuwa mwanafamilia wa Tanzania daima,ni wewe uliyenikutanisha na wafanyakazi wa Tanzania daima,kila nilipokuja Dsm,ilikuwa lazima nije Tanzania daima kuwasalimia.
Nilipoanza kazi Star TV,nilikushirikisha,ukanipa mawazo,umekuwa mshauri wangu,kila napomaliza kipindi ulikuwa unanipa feedback.
EDSON KAMUKARA,mara ya mwisho tulikaa meza moja Mlimani City tulipokwenda kupewa tuzo za umahiri wa habari,leo umekwenda,nakumbuka kabla hujaacha kazi Tanzania Daima na kwenda Mawio ulinipigia simu usiku,nikakwambia,"Oooooooh,unakwenda kumjoin Kubenea?".
Tukacheka sana,leo asubuhi nikakupigia simu,tukaongea kuhusu makala yako ya leo,tukacheka sana,leo jioni naambiwa umefariki dunia,Ooooh,EDSON KAMUKARA,umekwenda wapi mdogo wangu,nani atanipa feedback kila napomaliza kipindi EDSON?
Kweli umekwenda EDSON?nakulilia ,EDSON,Kila majadala wa kipindi cha jicho letu unapokuwa mgumu nilikuwa namuambia Mzee mpendu muite Kamukara na Balile hapa ndiyo mahali pao,sasa umetuacha,EDSON.
If possible amka my young brother,tulikupenda ila Mungu kakupenda zaidi,Tangulia Edson,ndugu,jamaa na rafiki zako tunakulilia,Ahsante Mungu kwa zawadi ya Edson,ulimleta na sasa umemchukua,Tangulia EDSON KAMUKARA.
0 maoni:
Post a Comment