HUU NI WARAKA WA CHAMA CHA MAPINDUZI







CHAMA CHA MAPINDUZI

MCHAKATO, MKAKATI NA MWENENDO WA KUFANIKISHA UCHAGUZI MKUU WA DOLA KWA NAFASI YA (RAIS, WABUNGE NA MADIWANI) KWA MWEZI OKTOBA, 2015 TANZANIA
IMEANDALIWA NA LT. MK MAGOVA (MST) WA JWTZ NA CCM.
WA => “LYASA, IMAGE, KILOLO, IRINGA TANZANIA”
TAREHE 08 JUNI 2015
1.0     UTANGULINZI:
Tanzania ni taifa lenye mfumo wa vyama vingi vya siasa kidemokrasia, kwa mujibu wa Katiba ya(Jamhuri ya muungano wa Tanzania) ya mwaka 1977 toleo la mwaka 1992 mpaka sasa 2015.
Mpaka sasa kuna vyama vya siasa 20 ambavyo vimesajiliwa kisheria kwa mujibu wa Katiba ya nchi na vyama vyote vilivyo na usajili wa kudumu wanayo haki ya kusimisha wagombea (Urais, Wabunge na Madiwani) katika mchakato huu wa uchaguzi wa mwaka huu wa Oktoba, 2015.

Watanzania tuko huru kwa mujibu wa Katiba ya nchi, kugombea nafasi yeyote ya (Urais, Ubunge na Udiwani) kwa kuzingatia sheria za Tume ya uchaguzi bila vurugu wala shari.Wagombea wote ni lazima wazingatie Katiba na Kanuniya Tume ya uchaguzi na sheria za nchi. Pia bila kuingilia shughuli za vyombo vya Dola vya ulinzi na usalama (JWTZ, JKT, POLICE, MAGEREZA, UHAMIAJI  NA FIRE BRIGED), wakati wa shughuli za uchaguzi na kuwaheshimu wapiga kura.

Vyombo vya habari,ni vyombo muhimu sana kutoa habari juu ya mwenendo wa chaguzi. Pia vyombo vya habari ni kupata habari toka kwa mihimili ya Dola na kupeleka habari kwa wananchi, ili kutoa habari kwa wananchi kwa kutumia (TV, Radio na Magazeti) ili kujua mchakato na mwenendo wa uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Waraka huu waelimishwe wana CCM kwa vikao au mikutano ya ndani.

2.0     MCHAKATO, MKAKATI NA MWENENDO WA UCHAGUZI:
2.1     Kwa mujibu wa Chama Cha Mapinduzi mchakato na mkakati wa mwenendo wa uchaguzi huazia kwa wanachama wa CCM kwa kutoa kura za maoni kwenye (Kata, Majimbo na Wilaya) na vikao vya kuwajadili wagombeawote waliogombea Urais, Ubunge na Udiwani kwa mujibu wa (Katiba na Kanuni ya uchaguzi) ndani ya CCM.

2.2      Vikao vya(Kamati ya maadili, Kamati ya sekretarieti, Kamati ya siasa, Halmashuri kuu na Mkutano mkuu) kwa ngazi ya Kata, Wilaya na Mkoa kwa kuwajadili (Wbunge na Madiwani) na kupendekeza kwenda ngazi za juu kwa uteuzi wa wagombea. Baada ya kuteuliwa watapambana na wagombea wa vyama vya upizani, kwa kunadi (Itikadi, Sera, Malengo, Mipango na Ilani) kwa kila Chama. Wananchi wataamua ni mgombea wa chama gani wanamtaka na kumchagua.

2.3     Kwa ngazi ya taifa kuna mchakato wavikao vya (Organazesheni, Sekretarieti, Kamati kuu, Halmashuri kuu na Mkutano mkuu) kwa ngazi ya taifa kwa kuwajadili wagombea Uraisbaada ya kudhaminiwa na wana CCM kwa zaidi ya mikoa 25 kwa (Tanzania bara na Zanzibar). Ndipo vikao hupendekeza na kuteua mgombea mmoja wa CCM kugombea Urais kwa kupambana na wagombeaUrais na vyama vya upizani. Wpiga kura watamchagua wanayemtaka kwa mujibu wa kukubalika kwa(Itikadi, Sera, Malengo, Mipango na Ilani) kwa Chama Cha Mapinduzi.

3.0     MAMBO YA KUZINGATI KWA WAGOMBEA WOTE WA (URAIS, UBUNGE
 NAUDIWANI) KWA CHAMA CHA MAPINDUZI:
3.1       Wananchi wakumbushwe mchakato wa historia ya utawala wa Tanzania.
A.      Tanzania ni taifa la muungano wan chi za (Tanganyika na Zanzibar) ambazo zote zilitawaliwa na wakoloni mbalimbali.
B.      Tanganyika na Zanzibar kulikuwa utawala wa kimila kwa kuongozwa na (Watemi, Watwa na Machifu)tangu mwaka 800 hadi mwaka 1885, wakoloni. Wajerumani walikuja mwaka 1880 na warabu waliingia  Zanzibar  tarehe 25/08/1896.
C.      Wananchi wazalendo wa Tnganyika walipinga wakoloni wa Ujerumani chini ya utawala wa Karl Peters, vilianza vita vya majimaji tangu tarehe 04/08/ 1905 hadi 1907 viliongozwa na Kinjikitile Bokero Ngwale kwa ukanda wa Ngarambe Matumbi. Walipigana (Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani, Morogoro na Iringa)
D.     Vita kuu ya kwanza ya Dunia walipigana tangu mwaka 1914 hadi mwaka 1918.
E.      Vita kuu ya pili ya Dunia walipigana tangu mwaka mwaka 1939 hadi 1945.
F.       Tanganyika ilitawaliwa na Wajermani tangu mwaka 1885 hadi mwaka 1919.
G.      Waingereza walitawala tangu mwaka 1920 hadi mwaka 1961.
3.2        Tanganyika kupata uhuru na Zinzibar kufanya mapinduzi.
3.3        Mchakato wa kujitawala watanzania, mpaka sasa ni juhudi za
wananchi wanzalendo wa kujitolea bila malipo mpaka sasa.
A.    TANU ilipigania (haki, usawa, uhuru na kujitawala) tangu mwaka 1954 hadi mwaka 1961, mpaka sasa tunaishi kwa amani na utulivu.TANU iliongozwa na (Mwalimu Julius Kambarage Nyerere)
B.    ASPilipigania (haki, usawa, uhuru na kujitawala)tangu mwaka 1857 na kufanya mapinduzi Januari, 1964 wananchi wazalendo walijitolea bila malipo kufanya mapinduzi dhidi ya utawala wa Sultan toka Oman.ASP iliongozwa na (AbeidAmani Karume).
C.     Kwa uongozi wa mwenyekiti wa TANU.Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Baba wa Taifa)na mwenyekiti wa ASP.Hayati Abeid Amani Karume. Walihamasisha wananchi wa(Tanganyika na Zanzibar) kuungana Aprili, 1964 na kuwa Tanzania hadi sasa.
D.    Vyama vya siasa vya TANUnaASPni vyama vilivyoandaa uimara wa CCM katika (kutawala, kuongoza na kusimamia kwa nidhamu vyombo vya ulinzi usalama) kwa manufaa ya umma wa Tanzania.
E.     CCM tangu kuanza kazi ya kutawala mwaka 1977 ni chama chenye historia katika ulimwengu kwa mambo yafutayo:-
1)      Kiliimarisha uchumi wa taifa katika sekta za (kilimo, ufugaji, uvuvi, viwanda, biashara na wajasiriamali)
2)      Kiliimarisha na kusimamia vyombo vya (ulinzi na usalama) kwa kulinda wananchi, mali na mipaka ya nchi(anga, maji na nchi kavu).
3)      Kiliimarisha sekta za (elimu, afya, mawasilano, nishati, madini na siasa)
4)      Kufundisha wapigania uhuru wa nchi mojawapo wa nchi za kusini mwa Afrika(Angola, Mozambiki, Zimbabwe, Namibia na Afrika Kusini) ili kujitawala kidemokrasia. Makamanda na wapiganaji wa jeshi la JWTZ  walikufamashuja 101kwa kusaidia Mozambiki na makaburi yako Nambele Mtwara. Kwa hiyo wananchi wajue hitoria ya CCM juuya amani na utulivu.
5)      CCM ilipigana vita vya Kagera (Tanzania na Uganda) kwa kuvamiwa na majeshi ya Uganda kwa kuongozwa na Nduli Idd Amin tarehe 25,10/1978 na mapambano ya vita yalianza rasimi kuanzia(Miziro, Mtukula na Kakuto) tarehe 22/01/1979  hadi tarehe 25/07/1978. Hadi kuwakomboa Waganda.
6)      Daraja la mto Kagera lilivunja tarehe 25/10/1978  na kujengwa hadi kukamilika tarehe 03/11/1978 na majeshi yaJWTZ  yalianza kuvuka na kuanza mapambano.
7)      Mojawapo wa makamanda wa vita vya kung’oa utawala wa Dikteta Nduli Idd Amin wa Uganda ni kama wafuatao:-
A.      Mwalimu Julius JK Nyerere alikuwa (Amiri Jeshi Mkuu) wa vita vya Kagera.
B.      Abud Jumbe Mwinyi alikuwa makamu wa kwanza wa Rais Tanzania
C.      Rashid Mfaume Kawawa alikuwa makamu wa pili wa Rais Tanzania.
D.      Edward Moringe Sokoine alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
E.       Jeneral Abdalah Twalipo Mkuu wa majeshi (JWTZ) wakati wa vita vya Kagera kati ya (Tanzania na Uganda).
F.       Jeneral David Msuguli alikuwa Kamanda mkuu wa vita mstari wa mbele.
G.     Brigedia Silas Mayunga –Mti Mkavu alikuwa Brigedi Kommanda wa 206 KV kwa upande wa Kakunyu kelekea Mbarara Uganda.
H.      Brigedia John Keats Walden alikuwa Brigedi Kommanda wa 207 KV Miziro kuelekea Masaka Uganda .
I.        Brigedia Mwita Chacha Marwa—Kambale Mamba alikuwa Brigedi Kommanda wa 208 KV upande wa Mtukula kuelekea Masaka Uganda.
J.        Kuna mafisa na wapiganaji walipigana vita vya Kagera usiku na mchana kwa (ushupavu na ujasiri) na walikufamashujaa 601 na kuzikwa Kaboya Bukoba Kagera, mpaka sasa familia za mashujaa hao wanaishi kwaa shida.
K.      Wananchi  waliandaliwa mafunzo ya Mgambo na JWTZili kwenda kupigana vita na majeshi ya kivita toka Uganda.

4.0          MCHAKATO NA MWENENDO WA VYAMA VYA SIASA TANZANIA:
4.1          Tanzania kuna mchakato wa historia wa vyama vya siasa tangu mwaka 1977
mpakaSasa mwaka huu wa 2015, lakini CCM ina mchakato ufutao:-
A.      Mwaka 1977 vyama vya TANU na ASP wanachama wa vyama hivyo walaamwua
kuunga na kuwa (CCM => CHAMA CHA MAPINDUZI) mpaka sasa ni chama tawala.
B.      Lengo la kuungana CCM na ASP ilikuwa ni kuimarisha (upendo, umoja, undugu,
mshikamano, uelewano, uzawa, uhuru, uzalendo na mahusiano bora)
C.      Kuimarisha masuala ya (amani, utulivu, ulinzi, usalama na kubinafasi).
D.     Kulaani, kukemea na kupinga masuala ya (siasa uchwara, udini, ukabila, ubaguzi wa
 rangi, ulevi wa madaraka, rushwa, hongo na takrima).
4.2       Tangu mwaka 1977 kulikuwa na mfumo wa chama kimoja tawalana kusimamia
vyombo vya ulinzi na usalama cha CCM hadimwaka1992.Ulipoanza mfumo wa
vyamavingi vya siasa mpaka sasa.
A.      CCM mwaka 1992 ilitoa maoni kwa wanachi wapige kura kuwa na mfumo wa vyama vingi au uendelee mfumo wa chama kimoja.
B.      Matokeo ya kura za maoni, wananchi 80% walitaka uendelee mfumo wa chama kimoja kutawala na wananchi 20% walitaka mfumo wa vyama vingi vya siasa.
C.      Mchakato wa vikao vya CCM vilianza kujadili na kufanya upembuzi yakinifu ili kufikia muafaka. CCMilimwita Mwalimu JK Nyerere (Baba wa Taifa)atoe maoni yake juu ya maoni ya wananchi. Alisema kuwa,kwa mujibu wa haki ya Demokrasia ni kwamba, wengi wape lakini kwa sasa duniani nchi nyingi kuna mfumo wa vyama vingi.Tanzania haiwezi kujitenga na mataifa kiuchumi na kisiasa. Kwa hiyo wananchi waelimishwe kuwe na mfumo wa vyama vingi vya siasa ili kuepukana na vurugu za watu wachache katika taifa, amani na utulivu ndani ya umma vitatoweka. Kwa hiyo wachache wanaopenda mfumo wa vyama vingi wakubalike.
4.3          Chaguzi kuu chini ya mfumo wa vyama vingi vya siasa tangu mwaka1995 hadi
uchaguzi wa mwaka 2010 ni kama ufutao:-
A.      Uchaguzi wa mwaka 1995 CCM kilipata 69% na vyama vya upizani walipata 31%, CCM kilishinda.
B.      Uchaguzi wa mwaka 2000CCM kilipata 71% na vyama vya upizani walipata 29%, CCM kilishinda.
C.      Uchaguzi wa mwaka 2005 CCM kilipata 82% na vyama vya upizani walipata 18%, CCM kilishinda.
D.     Uchaguzi wa mwaka 2010 CCM kilipata 61% na vyama vya upizani walipata 39%, CCMkilishinda.
4.4        Kwa mchakato huo wa mwenedo wa uchaguzi mkuu wa Dola tangu mwaka 1995 hadi
2010 Chama Cha Mapinduzi kilishinda. Je! Uchaguzi wa Oktoba,2015 ni chama kipi
kitashinda. Wana CCMni kuwa makini na hakuna kugawanyika na kukisaliti Chama Cha
Mapinduzi.Isipokuwa kwa kaulimbiu ya (umoja ni ushindi) izingatiwe.
4.5        Ushindi wa CCM kwa mwaka huu utatokana na kufanya vikao vya ndani kwa kutumia
jumuiya za CCM(WAZAZI, UWT na UVCCM) kuratibu takwimu za wapiga kura, wapenzi,
wakerketwa na washabiki wa CCM. Bila hivyo uchaguzi ni kulikoni ni lazima CCM kuwa
imara kwa kampeni.
5.0          CCM NI KUWA NA DHANA YA (UKWELI NA UWAZI)
5.1        Wajibu wa wagombea wa ngazi zote ni kueleza ukweli juu ya mapungu, matatizo, shida,
malalamiko na kero kwa wananchi (wakulima, wafugaji na wavuvi) wapewe maeneo ya
kufanyia shughuli zao za kilimo, mifugo na uvuvi. Siyo kuwanyang’anya maeneo yao na
kupewa wageni.
5.2       Wagombea kuwaeleza (wafanya biashara, wajasilia mali, mama lishe,machinga,
bodaboda, wasafirishaji wa ndege, meli, magari ya maroli na mabasi, mafuta, maji,
umeme, mawasiliano, na biashara nyingine) wazingatie sheria, za kulipa kodi na
kupewa maeneo ya biashara.
5.3       Wagombea kuwaambia haki zao (watumishi, wafanyakazi, walimu, madaktari, majeshi,
wastaafu, wazee, walemavu, wanawake wenye mimba, watoto, vijana kupata ajira,
matibau na dawa kuwa na ubora)
5.4       Wagombea kuwaeleza ukweli juu ya tuhuma zilizojitokeza juu ya wizi wa fedha za
wananchi(ESCROW, ITPL, RUSHWA WIZI na EPA) licha watuhumiwa kesi zao ziko
mahakamani na vyombo vya sheria.
5.5       Wananchi wawe makini sana kuwachagua viongozi ambao si waadilifu, pia viongozi wa
 TAMISEMI kuratibu takwimu mbalimbali  za(wazee, wanaume, wanawake, walemavu,
watoto, vijana, vifaa vya usafiri, zana za kilimo, ukubwa wa maeneo, mifugo, makazi,
kaya, idadi ya shule, vituo vya afya, zahanati, haspitali, mashamba,  na miundombinu
mbalimbali) kwa Tanzania uchumi mkubwa uko vijijini ambako kuna watu wengi sana.
5.6        Suala la uwajibikaji juu ya (usawa, haki za binadamu na utawala bora) ni jukumu la
mihimili ya Dola (Serikali kuu, Bunge na Mahakama) kutenda haki kwa wananchi.
Mihimili ya Dola siyo kutuhumiana na kashifa, hasa wakiwa bungeni, huo si utawala
bora ila ni ukiukaji wa maudhui na maadili katika taifa letu.
5.7        Wananchi wawe makini kuwachagua viongozi watakaokuwa makini juu ya kusimamia
mazingira na matibabu kwenye vituo vya afya na hospitali pia kunakuwa na dawa za
kutosha, ambazo zina kiwango chenye ubora. Pia viongozi watakaochaguliwa wawe
makini sana juu ya bidhaa feki zinazoingizwa kwa njia za panya.
5.8        Viongozi na watendaji waache masuala ya dhuluma na kutotenda haki kuwalipa watu
sitahil zao iwapo fedha zitatolewa na serikali kwa shughuli za maendeleo ya jamii,
malipo ya safari na uhamisho au malipo kwenye matibabu.
5.9        Wananchi wawachague viongozi watakaosimamia haki za mahakama kuhukumu
mapema watu wenye makosa ya jinai, kuliko watu kulundikana mahabusu zaidi ya miaka
mitano bila kuhukumiwa, serikali inazidi kujenga Magereza kwa gharama. 

A.      MWISHO WANANCHI WAAMBIWE KWAMBA:-
B.      Serikali ni wananchi au umma ndio wanaolipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
C.      Hazina na BoT ni haki ya wananchi ambao hulipa kodi na VAT si haki ya mihimili ya Dola, fedha ni kwa ajili ya maendeleo na kujenga miundombinu mbalimbali kwa wananchi.

D.     Wananchi waambiwe kwamba(nchi na watu ni taifa) bila nchi na watu hakuna taifa. Kwa sasa kuna baadhi ya viongozi na watendaji hawajali kusimamia taifa katika masuala ya maendeleo, kwa manufaa ya taifa.
E.      Wananchi wawe makini kuangalia mali asili kama vile (wanyama, misitu, ndege, madini, maji na mazingira)ni jukumu la wananchi sehemu zao hasa vijini.
F.       Wananchi wawe makini kwa wagombea wanaotoa rushwa, hongo na takrima hawana sifa ya kuwaongoza wananchi katika taifa letu ila wana sifa ya kuhujumu uchumi.
G.     Wananchi wawe huru kuchagua kiongozi anayekuwa karibu na wanachi kwa kusikiliza na kupokea kero zao na ushauri  wakati wote siyo viongozi wa kushinda kwenye Baa hafai.
H.     Watanzana wote wajue kwamba, amani (haicheziwi, haikosewi na haijaribiwa) kwani amani ikitoweka ni(majuto, kufa, kuhangaika na kuimbia nchi yako) watu wote ni (kufikiri, kutafakari na chambua) nini maana ya (usawa, uhuru, uzalendo, demokrasia, kubinafasi, haki za binadamu na utawala bora) katika taifa letu la Tanzania vitazingatiwa.

+Kaulimbiu yetu tunahitaji (amani, siri, miiko, utulivu, upendo, mshikamano, umoja, uelewano, kukubaliana, ulinzi na usalama)ni kuzingatia wakati wa uchaguzi bila vurugu wala shari+

                                           --------------------------------------------
Lt Mberito Kimvelye Magova (mst)
(MBEKIMA)
KADA WA ELIMU YA JAMMI


=MUNGU IBARIKI TANZANIA, AFRIKA NA ULIMWENGU KWA UJUMLA=

0 maoni:

Post a Comment