LOWASSA APATA WADHAMINI ZAIDI YA 3000-GEITA

Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa,(katikati), akipungia mkono maelfu ya wana CCM na wananchi wengine waliofika kwenye ofisi za CCM wilayani Geita Juni 8, 2015, kwa nia ya kumdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015; (Picha zote na K-VIS MEDIA)
Wakazi wa wilaya ya Geita, wakiwa juu ya nyumba na juu ya mti (picha ya chini), ili kumuona Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa, alipowasili kwenye ofisi za CCM wilayani Geita, Juni 8, 2015 kuomba wana CCM wamdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Umati wa wana CCM waliofika kumdhamini Lowassa, na ananchi wengine waliofika walau kumuona wakiwa wamefurika nje baada ya ukumbi wa mikutano ofisi ya CCM wilayani Geita “kutapika”.
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge a Monduli, Mh. Edward Lowassa, akipokea fomu za udhamini za CCM baada ya kujazwa na wananchama wa CCM wilaya ya Geita, kwenye ukumbi wa CCM wilayani humo Juni 8, 2015. Mheshimiwa Lowassa, amedhaminiwa na jumla ya wanachama 3,000 wilayani hapo.
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Losassa, akiwaaga wananchi na WanaCCM waliofika kumdhamini kwenye ofisi za CCM wilaya ya Chato Juni 8, 2015.
Lowassa akiteremka kutoka ndani ya ndege, kwenye uwanja mdogo wa ndege wa mgodi wa Geita (GGM)
Lowassa, akiwapungia wana ccm waliofika kumdhamini baada ya kukabidhiwa fomu za udhamini zilizojazwa. Jumla ya wana CCM 3,000 walijitokeza kumdhamini.
Wana CCM waliofurika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za chama hicho ilayani Geita, wakimshangilia Lowassa.
Lowassa, akiondoka huku akiwa amezungukwa na umati wa watu nje ya ofisi za CCM wilayani Geita.

0 maoni:

Post a Comment