Nia
ya kuwania nafasi ya uraisi imezidi kuendelea ambapo leo Aliyekuwa waziri
nishati na madini wa awamu ya nne Mh William Ngeleja ametangaza nia ya kuwania
nafasi uraisi katika Uchaguzi mkuu wa Mwaka huu.
Akitangaza
nia yake mbele ya waandishi wa habari na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi
katika ukumbi wa Benki kuu ya Tanzania,Jijini Mwanza Mheshimiwa Ngeleja amesema
kuwa dhamira kweli aliyonayo ni kupambana na umasikini, ujinga, maradhi, rushwa,
ufisadi, na mmomonyoko wa maadili ndani ya nchi.
Ngeleja ametaja sifa za raisi ambaye watanzania wanataka
atakayepambana na maadui wakubwa wa nchi ambao ni rushwa, umasikini, ujinga,
maradhi, ufisadi na mmomonyoko wa maadili pia atakaye simamia kwa dhati umoja
na mshikamano wa Taifa,muungano na kuilinda amani ya nchi,kukemea kwa nguvu
ubaguzi wa rangi,dini, na kikabila, Kuimarisha usalama na ulinzi wa nchi.
Ambapo
amesema kuwa shauku yake kubwa katika uongozi wake atakaopewa na watanzania ni
kuwakomboa wakulima, wavuvi, wafugaji, wachimbaji, wadogo wa madini,
wajasiriamali, wasanii na wanamichezo n.k ambao ndio kundi zima la wananchi
masikini.
Ili kulinda mafanikio ya nchi yaliyopo na yatakayoachwa na awamu iliyopita
inapaswa kuzilinda na kuzisimamia rasilimali zilizopo sasa kwa manufaa ya
watanzania na kuzikabili changamoto zilizopo na zijazo Tanzania inahitaji
uongozi makini imara unaohimili misukosuko mitihani na majaribu ya kila aina.
Amewaambia
watanzania kuwa amejiandaa kwa moyo wote kupokea majukumu atakayoachiwa na raisi
aliyepo madarakani kwa sasa Dokta Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuwa amejipima na kuona anafaa kuwatumikia na kuwaongoza watanzania katika ngazi ya uraisi wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.
Mh William
Ngeleja amekuwa kiongozi wa 12 kutoka Chama Cha Mapinduzi kutangaza nia ya
kugombea nafasi ya urais.
Via
Star TV/Yohana Emmanuel
0 maoni:
Post a Comment