Rais Jakaya Kikwete amesema serikali yake itaendeleza mapambano dhidi ya kundi la watu wasio na utu wanaoua na kuwajeruhi watu wenye UALBINO nchini kwa madai ya kutafuta utajiri ili kuhakikisha kuwa walemavu hao wanaishi maisha ya amani kama katiba ya nchi na mikataba ya kimataifa inavyoelekeza.
Akizungumza ma maelfu ya wananchi waliohudhuria maadhimisho siku ya watu wenye UALBINO duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Arusha Rais Kikwete aliyeonyesha kuguswa na ujumbe uliofikishwa na watoto wenye UALBINO kwa njia ya nyimbo amesema ni kwa kutambua kuwa vitendo hivyo vimekua vikichochewa na imani za kishirikina serikali yake ililazimika kupitia upya baadhi ya sheria hususani zile zinazolinda maslahi ya watu wenye ulemavu.
Maadhimisho hayo yalitanguliwa na dua kutoka kwa viongozi wa dini ambao wote kwa pamoja wanakemea unyanyasaji unaofanywa dhidi ya walemavu hao.
Kilio chao kingine cha watu wenye ualbino upatikanaji wa huduma ya afya stahiki.
Katika hilo mwakilishi mkazi wa umoja wa mataifa nchini Alvaro Rodrguez anasema wanashirikiana na serikali kuhakikisha kuwa kundi hilo linapata huduma huku wizara ya afya ikisema tayari imeshajenga mazingira mazuri ya upatikanaji wa mafuta ya kuzuia mionzi ya jua inayosababisha saratani ya ngozi.
0 maoni:
Post a Comment