WAKULIMA MBARALI,MBEYA WATOA YA MOYONI WANAYOKUMBANA NAYO KATIKA KILIMO CHA MPUNGA

WAKULIMA wa zao la Mpunga kwenye bonde la Usangu Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wamesema matumizi ya mbegu za mpunga zisizo na ubora zinachangia kwa kiasi kikubwa  kupata mavuno yasio na tija na kushuka kwa soko  huku wakilalamikia ujazo la rumbesa kwa gunia.
 
Wamesema haya wakati wa siku ya Mkulima, iliyoandaliwa na Kampuni ya Mtenda Rice Supply inayojishughulisha na masuala ya Kilimo Mkoani Mbeya ambapo wanasema ikiwa watapata elimu ya kutosha  juu ya mbegu bora za mpunga kilimo chao kitakuwa na tija.
 
Aidha Mkurugenzi wa Kampuni ya Mtenda Rice Supply, George Mtenda amewataka wakulima kuorodhesha majina yao mapema Septemba mwaka huu ili waweze kupata elimu ya matumizi ya mbegu bora na kilimo cha kitaalamu, pamoja na kukopeshwa pembejeo za kilimo.
 
Hata hivyo katika bonde hili vijana wengi wanajihusisha na kilimo cha mpunga ambapo wameshauri vijana wengine kujikita kwenye kilimo na kuacha tabia ya kukimbilia mijini.

0 maoni:

Post a Comment