WAZO LANGU MTU HURU KWAKO MWENYE LOLOTE

Ninachokifahamu mimi kwamba; Dunia ina fedha nyingi mno za kutengeneza, huna sababu ya kugombana na mtu, kumchukia au kumnunia mwingine sababu ana kitu fulani ambacho wewe huna! Cha kufanya ni kutumia akili yako kuwaza na kuwazua ukitafuta majibu ya malalamiko ya watu, kamwe na wewe usijaribu kuwa mlalamikaji kama walivyo asilimia kubwa ya watu(hasa sisi)nikisema sisi nadhani umenielewa; Watalaam wa kuketi vijiweni, mitandaoni bila kufanya chochote, tukiongelea watu. Huwezi kufankiwa maishani kama huo ndio mtindo wako wa kuendesha mambo ni lazima ubadilike.
Ndugu zangu,
Asilimia 2 ya watu Dunia walioamua kuwa sehemu ya watafuta majibu na si sehemu ya walalamikaji waliishia kufanikiwa sana kifedha, kumbe basi cha Muhimu katika maisha ya mwanadamu ili afanikiwe ni wazo, si wazo tu bali wazo bora la biashara, si fedha! Nasema hivi sababu karibu kila kijana ninayekutana nae nikimuuliza nini sababu uko hivi? Jibu limekuwa lile lile "mtaji" neno hili ndilo limekuwa sababu ya vijana wengi kubaki na walipo na kutoingiza ubongo kazini.
Nimesema mara nyingi na leo narudia; WAZO NI BORA KULIKO MTAJI! Nilipoanza biashara rasmi mwaka 1998, sikuwa na mtaji wa fedha bali nilikuwa na wazo ambalo miaka kumi na sita baadae kila nilichokihitaji wakati ule ninacho, hii ina maana nyumba, gari, mwanamke mzuri, Heshima nk, vyote vipo ndani ya Wazo! Vipi kama ningebaki mlalamikaji? Ningekuwa hapa leo? Chukua hatua.
Binafsi Nililiamini wazo langu nikapuuza maneno ya watu na kusonga mbele, hata wewe Ukifanya hivyo utahama kwenye asilimia 98 ya watu walalamishi wasio na mafanikio na kujiunga na asilimia 2 ya watafuta majibu wenye mafanikio.
KILA MMOJA WETU ANAWEZA KUFANYA VIZURI KIFEDHA MAISHANI, USIDANGANYWE NA MTU YEYOTE KWAMBA KUFANIKIWA KIFEDHA NI KWA KUNDI FULANI NA WATU. UKWELI NI KWAMBA ASILIMIA TISINI YA MATAJIRI DUNIANI WALITOKEA KWENYE UMASIKINI, UNACHOTAKIWA NI KUFANYA CHAGUO NA MAAMUZI SAHIHI KISHA KUKUBALI KUHANGAIKA NA WAZO LAKO LA BIASHARA UKIWA UMEKATAA KUKATA TAMAA MPAKA UPATE UNACHOKITAKA. HIKI NDICHO MATAJIRI WOTE WALIFANYA NA NDIO MAANA WAPO WALIPO.
Hakuna kitu kinanikera kama kufundisha watu vitu lakini hawavifanyii kazi na matokeo yake wanabaki walivyo, katika maisha yangu nimejitahidi kujianika ili watu wajifunze na maisha yao kubadilika lakini cha kushangaza asilimia kubwa ya watu hawafanyii kazi mafundisho yangu,wengine wanahudhuria katika kila semina yangu lakini hawasongi mbele, inaniumiza na kunisikitisha sana.
Wengine hata kwenye hawahudhurii, wakiulizwa jibu lao ni; yule hnancha kuniambia mi GRADUATE! Graduate????? Ndugu yangu achana na mambo ya unanizidi elimu au mimi sio profesa kama waliokufundisha chuo kikuu hivyo sina jipya, ni kweli! Nakusihi uchukue muda uangalie mambo niliyoyafanya hapa duniani kisha chukua mazuri yangu na mabaya niachie mwenyewe. Nakuhakikishia kwa kufanya hivi utafanikiwa sana, hasa kwa sababu wewe una elimu kubwa ya darasani kukiko mimi, cha muhimu uachane na "ego" ama majidai ya kiwango chako cha elimu ambacho kimegeuka Gereza na uwe tayari kujifunza na kufanyia kazi ulichofunza.
Ndugu yangu,
Acha nikuage kwa kukupa wazo la biashara ambalo nina uhakika litakufanya kuwa bilionea hapa duniani, ni wazo ambalo mimi nililigundua miaka mingi iliyopita na kwa kweli nilitaka kufanya mwenyewe, lakini kwa jinsi nilivyo na kazi nyingi kwa sasa, nakiri siwezi tena kulitekeleza na kwa sababu hiyo basi ni vyema nikupe wewe ulifanyie kazi na likunufaishe wewe na taifa letu kwa ujumla.

0 maoni:

Post a Comment