Hapa ni katika ukumbi wa mikutano wa NSSF mjini Shinyanga ambako leo kwa mara kwanza mkoani Shinyanga Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania imefanya mkutano mkubwa wa Amani,huku watu wa kada mbalimbali wakihudhuria mkutano huo wakiwemo viongozi wa jumuiya,madhebehu mengine ya dini,vyama vya siasa,serikali,vikundi maalum vya watu katika jamii na wananchi mbalimbali wenye mapenzi mema.
Mgeni rasmi alikuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga.Mutano huo ulikuwa na lengo la kuwahamasisha na kuwaomba wananchi wote waislamu na wasio waislamu kuishi kwa misingi hiyo ambayo inakubalika na kila mtu muungwana.Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,ndugu Kadama Malunde,ametuletea picha 30 za mkutano huo,Angalia hapa chini
Awali Sheikh Waseem Khan akisoma Quran Tukufu(dua) wakati wa mkutano huo ambao umefanyika kwa mara ya kwanza mkoani Shinyanga na mara ya pili kanda ya ziwa Victoria
Mkutano huo umeandaliwa na Jumuiya ya waislamu ya Ahmadiyya Tanzania ambayo ipo hapa nchini kwa zaidi ya miaka 80,ukiwa na lengo la kuhimiza umuhimu wa amani katika nchi ya Tanzania
Naibu katibu mkuu wa Jumuiya ya waislamu ya Ahmadiyya Tanzania Ustaadh Abdulrahman Ame akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema kauli mbiu yao ni "Love For All Hatred For None",yaani "Upendo kwa wote bila chuki kwa yeyote",ana kwamba wamekuwa wakihubiri kwa upendo na amani bila kuleta kashfa wala chuki dhidi ya imani au madhehebu yoyote
Viongozi wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania wakiongozwa na Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhiry walisema sera ya Jumuiya hiyo kama zilivyo sera za jumuiya zingine za kidini duniani kote ni kutojiingiza katika masuala ya kisiasa ya nchi yoyote,isipokuwa waumini wao wanaweza kushiriki katika siasa za nchi zao katika ngazi ya mtu binafsi
Mgeni rasmi katika mkutani huo,mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akizungumza katika mkutano ambapo alisema katika kipindi hiki ambacho taifa linaelekea katika uchaguzi ni muhimu kwa jumuiya za kidini kubaki na majukumu yao ya msingi pamoja na kuhubiri amani pasipo kuchanganya masuala ya imani na siasa.
“Ili kudumisha amani ya nchini ni vyema Jumuiya za dini zibaki na majukumu yao ya msingi na kuhubiri amani ili waumini wa dini mbalimbali wawe huru kuwachagua viongozi wanaowapenda huku wakiendeleza umoja wao kwenye dini na imani zao”,alisema Rufunga.
Tunafuatilia kinachoendelea.....
Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania mbali na kuhubiri amani katika maeneo kadhaa pia huwa inatoa misaada ya kijamii,na hivi karibuni Jumuiya hiyo ilitoa msaada kwa wahanga wa mvua ya ajabu ya Mwakata huko wilayani Kahama
Kiongozi wa mkutano huo Yusuph Mgeleka akisisitiza jambo katika mkutano huo wa kihistoria mkoani Shinyanga
Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhiry akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka viongozi nchini kuwa waadilifu kwa watu wanaowaongoza huku wananchi nao wakitakiwa kuwa waadilifu kwa mamlaka za nchi zao na baina yao ili kudumisha amani ya nchi.
Kundi la watu wenye ulemavu wa ngozi wakifuatilia mkutano huo wa amani
Akizungumza katika mkutano huo mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga alisema Mkoa wa Shinyanga una baadhi ya matukio ya uvunjifu wa amani na uhalifu kama vile mauaji ya vikongwe na albino hivyo kutoa wito kwa viongozi wa serikali,dini na vyama vya siasa kuendelea kuhubiri amani ndani na nje ya mkoa huo ili kuondoa kabisa imani zisizo na tija katika mkoa wa Shinyanga
Rufunga alitumia fursa hiyo kuwasisitiza watanzania kuvumiliana na kuheshimiana miongoni mwa wanadini na waumini wa imani mbalimbali.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Shinyanga ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine Matiro akizungumza katika mkutano ambapo alisema suala la kuimarisha amani ni jukumu la kila mtu katika jamii hivyo kuwataka wananchi kutoa taarifa kwa vyombo vinavyohusika pindi wanapoona kuna dalili za kutokea uvunjifu wa amani
Mwakilishi wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,mrakibu msaidizi wa polisi Hatari akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema kila mtu ana jukumu la kulinda amani ya nchi kisheria
Mkutano unaendelea
Mkuu wa vikosi vya Jeshi la Wananchi (JWTZ) mkoa wa Shinyanga Kanali Musa Kingay akizungumza umuhimu wa kutunza amani ya nchi katika mkutano huo
Kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Shinyanga Inspekta Elisa Mugisha akizungumza katika mkutano huo wa amani
Kushoto ni Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Emmanuel Makala akizungumza katika mkutano huo wa amani ambapo alisema amani ya nchi itaendelea kuwepo endapo viongozi wanaoongoza nchi watatenda haki kwa wananchi wanaowaongoza.
Mwakilishi wa Bakwata mkoa wa Shinyanga Sheikh Alhaj Alley Juma akizungumza katika mkutano huo wa amani
Mkutano unaendelea
Mwakilishi wa askofu wa jimbo katoliki la Shinyanga,Padre Dustan Sitta akizungumza katika mkutano huo kwa niaba ya mhashamu askofu Liberatus Sangu
Mkutano huo ulienda sambamba na kuombea mkoa wa Shinyanga na taifa kwa ujumla
Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania ina kiongozi mmoja duniani ambaye moja ya jukumu lake kubwa ni kujitahidi kuwaomba wanadamu kuishi kwa kuzingatia misingi ya amani
Tunafuatilia kinachoendelea ukumbini....
Baada ya mkutano baadhi ya viongozi wakaamua kupiga picha za kumbukumbu
Picha ya pamoja
Picha ya kumbukumbu,mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro,mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga na Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhiry .
0 maoni:
Post a Comment