
Mwili wa mwandishi wa habari Edson Kamukara umezikwa jana Juni 29,2015 katika kitongoji cha Bukujungu,Ihangiro wilayani Muleba,huku wale waliopata nafasi ya kutoa salamu za rambi rambi wakiweka wazi kuwa chanzo cha kifo chake bado ni utata na kwamba kimetokana na kazi yake ya uandishi wa habari.
Akizungumza katika maziko hayo, mkurugenzi wa kampuni ya mwana halisi publishers LTD Bwana Said Kubenea, alisema kifo cha marehemu Kamukara, kimezua utata kutokana na hakuna anayejua undani.
Alisema kuwa madakatari wanasema inaonekana alikufa baada ya kukosa hewa huku, chumbani kwake kukikutwa na damu, huku akiongeza kuwa Edson alikuwa anakamilisha kazi ya uandishi uliokuwa ukiwahusu vigogo na kama habari zake zingetoka, saivi nchi ingekuwa inaongea mambo mengine.
Edson Slavatory Kamukara, amezikwa kijijini kwao Ihangiro wilayaniMuleba, huku akiacha majonzi kwa familia yake, baada ya kuacha mtoto mmoja ilhali mama yake akisumbuliwa na kupooza, ambapo siku chache zilizopita, Edson alitokea Muleba kumuangalia mama yake, kama alivyozungumza dada wa marehemu aliyejulikana kwa jina la Joyce.
Marehemu Edson Kamukara, ameacha mtoto anakadiriwa kuwa na miaka kati ya 3 hadi 4 aitwaye Edgar Ishengoma, na marehemu alianza kazi ya uandishi katika gazeti la Majira, akafanya Jambo leo, Tanzania daima, na hatimaye mwanahalisi publishers ambapo amefanyia kwa kipindi cha miezi minne, na alikuwa anakamilisha habari kuhusu matatizo ya wananchi kupitia viongozi mkoani Kagera.
ANGALIPA PICHA HAPA CHINI KUTOKA KIJIJINI ALIKOZIKWA
Mwili wa aliyekuwa Mhariri wa Kampuni ya Mwanahalisi, Edson Salvatory Kamukara aliyefariki alhamisi ya wiki iliyopita jijini Dar es Salaam umezikwa jana Nyumbani kwao Muleba mkoani Kagera katika Kijiji cha Ihangiro kitongoji cha Bukujungu na kuagwa na mamia ya waombolezaji.Marehemu Edson alizaliwa 27,03.1980 na kufariki wiki iliyopita juni 25, 2015 na amezikwa Jumatatu Juni 29, 2015. Marehemu walizaliwa Mapacha na ameacha Pacha mwenzake Edda na ameacha Mtoto wake anayeitwa Edgar.







Dada yake mkubwa na marehemu Joyce akisoma kwa ufupi historia ya Marehemu Mdogo wake Edson Salvatory Kamukara,

Umati mkubwa wa Watu walijitokeza kumuaga.





0 maoni:
Post a Comment