HOFU YA EBOLA TENA DRC

Watu wanne wamefariki dunia wakiwa na dalili za ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.


Mamlaka za Afya nchini humo zinachunguza uwezekano wa kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa huo.
Waziri wa Afya Felix Kabange amesema wafanyakazi wa afya wamepelekwa katika kijiji cha Masambio kilichoko kilomita 270, kaskazini mwa mji mkuu wa nchi hiyo Kinshasa, kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Amesema wawindaji sita walipatwa na homa Ijumaa iliyopita wakiwa na dalili za ugonjwa huo, ikiwemo, kuhara na kutapika baada ya kuua na kula Paa.
Waziri huyo wa afya hata hivyo amesema kati ya hao, wakiwemo wanne waliofariki hakuna aliyeshikwa na homa kali, dalili ambayo ni ya mwanzo na kubwa ya ugonjwa huo.

0 maoni:

Post a Comment