Mgombea mwenza wa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
Baada ya kutangazwa kuwa Magufuli ndiye atapeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu ujao,Mheshimiwa John Magufuli akazungumza kisha kumteua mgombea mwenza katika uchaguzi mkuu ujao 2015.
"Napenda kumshukuru mwenyezi mungu kwa kunifanya niwe salama...Nimehewa nafasi mliyonipa ni kubwa sana....Jana wakati naomba kura niliwaambia nitumeni nami nitawatumikia...nitawatumikia kwa nguvu zangu zote,kwa moyo wangu wote, kwa kutumia vipaji vyangu vyote nilivyopewa na mwenyezi mungu...wingi wa kura hizi nilizopata ni uthibitisho kuwa CCM ni wamoja...naamini tutashirikiana ili kuutafsri ushindi huu katika uchaguzi mkuu ujao"- Dkt Magufuli.
"Kinachotakiwa ni ushirikiano kwa wanachama,wote,tuungane kwa pamoja ili kuhakikisha kuwa chama chetu kinapata ushindi ulio mnono sana kwenye uchaguzi mkuu ujao...Nafurahi kuwa napeperusha bendera ya chama imara,chenye watu wenye hamasa kubwa ..,chama kilichoipatia sifa nzuri nchi yetu,chama kilicho komaa"- Dkt Magufuli.
"Waheshimiwa wanachama wenzangu wa CCM naomba kuwahakikishia kuwa nitakuwa nanyi kweli kweli,nitakuwa mtumishi wenu...hapa ni Chama Kwanza,nawahakikishieni Ushindi mkubwa katika uchaguzi ujao"-Dkt Magufuli.
"Nimekaa na kufikiria..imeamua kumteua mgombea mwenza wangu awe Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan,Baada ya kusema haya naomba tushirikiane ili CCM ipate ushindi,asanteni sana!!"- Magufuli.
Mkutano mkuu wa CCM umefungwa na mwenyekiti wake Dkt Jakaya Kikwete,kinachofuata sasa ni mkutano wa kumtambulisha mgombea huyo leo mkoani Dodoma katika uwanja wa Jamhuri na kesho kutwa siku ya Jumanne mkutano wa hadhara wa kumtambulisha Dkt Magufuli utafanyika jijini Dar es salaam.
Akifunga mkutano huo,mwenyekiti wa CCM taifa Rais Jakaya Kikwete amemmwagia sifa kem kem Dkt Magufuli kutokana na uchapakazi wake,ubunifu na misimamo yake katika mchakato wa maendeleo hivyo kuwaaminisha wanaCCM na watanzania kwa ujumla kuwa Magufuli anafaa kuiongoza nchi ya Tanzania kutokana na uwezo mkubwa alionao.
Rais Kikwete amewataka wanaccm kuvunja makundi yao na kuungana pamoja na kuwa kitu kimoja ili kutafuta ushindi wa CCM.
"Magufuli na Samia Suluhu wanauwezo mkubwa wa kufanya kazi...Kinachotakiwa sasa ni kutafuta Ushindi wa CCM,Siyo Magufuli...,wagombea walikuwa wengi sana lakini amebaki mmoja,Tunahitaji ushindi kuanzia Udiwani,Ubunge na Rais...tutengeneze mikakati dhabiti...Nawatakieni safari njema ya kurudi makwenu,kazi mnayotakiwa kufanya ni kuitafutia CCM ushindi"_ Kikwete
0 maoni:
Post a Comment