Maelfu ya wakazi wa Geita wakimlaki Dkt Magufuli
Dkt Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Geita
Mkoa wa geita na viunga vyake umezizima kwa muda wakati mgombea wa kiti cha urais wa chama cha mapinduzi (CCM)Dk.John Pombe Magufuli alipokuwa akitambulishwa na kuagwa na wapigakura wake wa jimbo la Geita huku wananchi wakimtaja kama mkombozi wa kulivusha taifa kuelekea katika haki na usawa kwa watanzania wote.
Akiwa njiani kutokea mkoani mwanza kuelekea mkoani geita katika eneo la chato alikozaliwa msafara wa dr magufuli ulijikuta ukisimamishwa njiani mara kwa mara na umati mkubwa wa wananchi bila ya kujali jinsia na rika waliojitokeza barabarani kwa lengo la kutaka kumuona huku wakiwa na matawi ya miti.
Akitambulishwa na umati mkubwa wa wananchi katika ofisi za mkoa wa chama hicho mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Joseph Msukuma Kasheku amesema chama hicho hakika hakikukosea kumteua Dr. Magufuli kugombea nafasi ya urais kupitia chama hicho kwa kuwa ni kipenzi cha watanzania wote bila ya kujali itikadi za kivyama.
Akizungumza wakati akiwashukuru,kuwaaga na kujitambulisha kwa wananchi waliokusanyika katika ofisi za chama cha mapinduzi mkoani Geita na hatimae vunja jungu katika jimbo la Chato mgombea urais wa CCM Dr.John Pombe Magufuli amekishukuru chama hicho kwa kumuamini na kuongeza kuwa makundi ya wagombea wa nafasi ya urais ndani ya chama hicho yamezikwa rasmi na limebaki kundi moja la umoja ni ushindi.
Wakizungumzia uteuzi wa Dr.Magufuli kugombea kiti hicho cha urais kupitia Chama Cha Mapinduzi baadhi ya wananchi wamesema tanzania imepata kiongozi atakayesaidia kuipeleka tanzania katika nchi ya ahadi.
0 maoni:
Post a Comment