Zaidi ya Nusu ya kata katika Jimbo la Tabora Mjini zimevuka lengo la kuandikisha wapiga kura kwa zaidi ya asilimia moja huku kata mbili zikifikia lengo la kuandikisha wapiga kura kwa asilimia mia moja,Kata zilizovuka lengo ni 18 kati ya Kata 29 zilizopo Jimbo hilo huku wastani wa uandikishaji ukiwa ni asilimia 105 kwa kata zote 29.
Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Tabora Mjini,Sipora Liana,amesema,watu waliokadiriwa kuandikishwa ni 130,686 huku idadi kamili ya walioandikishwa ikifikia watu 137,542.
Katika zoezi hilo lililoanza tarehe 21 May kwa awamu nne ,ukiwa na siku saba kwa kila awamu ulikabiliwa na changmoto kadhaa ambazo zinatajwa na Sipora Liana kuwa ni pamoja na kuharibika mara kwa mara kwa mashine za BVR , upungufu wa vifaa uliojitokeza ambavyo ilibidi kuagizwa kutoka Tume ya taifa ya uchaguzi na baadhi ya wananch kutotaka kusubiri hadi kipindi cha kujiandikisha katika eneo lake kifike.
Amebainisha kwamba utatuzi wa changamoto hizo ulifanyika kwa wataalamu kujitahidi kuzifanyia matengenezo mashine wakati wote hadi usiku wa manane huku vituo vilivyoshindwa kukamilisha uandikishaji ndani ya siku saba vikiongezewa muda.
Sipora amesema mafanikio yamepatikana kutokana na ushirikiano kati ya Ofisi yake na Vyama vya Siasa vilivyopewa jukumu la uhamasishaji,ushiriki wa Viongozi wa Serikali katika uhamasishaji,Ushirikiano kati ya ofisi yake na wasaidizi wake pamoja na uwezo mzuri wa wataalamu wa IT waliopelekwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Jimbo la Tabora Mjini lina idadi ya vituo vya kujiandikisha wapiga kura vipatavyo 222 ingawa wadau walipendekeza viongezeke hadi kufikia vituo 294 lakini hawakukubaliwa.
0 maoni:
Post a Comment