PICHA ZA LIONS CLUB INTERNATIONAL IKITOA MSAADA WA MADAWATI MKOANI SHINYANGA




Chama cha Kimataifa kinachotoa misaada mbalimbali ya Kijamii cha Lions Club International chenye makao yake makuu nchini Marekani leo kimetoa msaada wa madawati 100 ya chuma yenye thamani ya shilingi milioni 9,katika shule ya msingi Town iliyopo mjini Shinyanga ili kuondokana na changamoto ya uhaba wa madawati kwa shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 1019.

Akizungumza wakati wa kukabidhi madawati hayo mia moja ya chuma,mwenyekiti wa Lions Club International katika nchi ya Uganda na Tanzania kupitia tawi la Mwanza bwana Lion Patel Yogesh amesema wameamua kutoa msaada huo ili kuondoa changamoto ya madawati katika shule hiyo iliyopo katikati ya mji wa Shinyanga.

Yogesh amesema Lions Club pia italeta madawati mengine 164 sambamba na kupaka rangi majengo ya shule hiyo kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu ili kuyafanya mazingira ya shule hiyo kuwa rafiki kwa wanafunzi.

Awali mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam aliyetafuta wafadhili hao akiwa miongoni mwa wanachama wa Lions Club,amesema ataendelea kutafuta wafadhili ili kuondokana na changamoto mbalimbali katika shule za manispaa ya Shinyanga.

Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo iliyojengwa mwaka 1942 ,Josephine Mabula amekishukuru chama hicho kwa kutoa msaada huo na kupongeza juhudi za meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam kwa kutumia muda wake mwingi kutafuta wafadhili kusaidia shule za manispaa ya Shinyanga.

Pamoja na msaada huo wa madawati 100,Lions Club pia imekabidhi Computer Mpakato 3 kwa shule ya sekondari Town,Old Shinyanga,Kizumbi kwa ajili ya kutunzia kumbukumbu mbalimbali na shilingi laki moja kwa chuo cha Ualimu Shycom kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa bweni unaondelea.

Wakati huo huo Chama cha Kimataifa Lions Club International leo kimetoa msaada chakula katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa Ngozi cha Buhangija ili kuwapunguzia changamoto kubwa ya chakula.




Wanafunzi wa shule ya msingi Town mjini Shinyanga wakiimba wimbo wakati wa kupokea madawati hayo ya 100 ya chuma walipewa na Chama cha Kimataifa kinachotoa misaada mbalimbali ya Kijamii cha Lions Club International kupitia tawi lao Mwanza 

Viongozi mbalimbali wa Lions Club wakiwa katika shule ya msingi Town mjini Shinyanga 

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Town bi Josephine Mabula akisoma risala kwa mgeni rasmi ambaye ni mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga ndugu Gulam Hafidh Mukadam.Katika risala yake alisema shule yake ina jumla ya wanafunzi 1019 na changamoto kubwa sasa ni madawati na baada ya kupatiwa madawati 100 pungufu sasa ni madawati 164.

Kushoto ni meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam,akifuatiwa na mwenyekiti wa Lions Club kanda ya ziwa bwana Lion Parimal Patel,kulia ni bwana Lion Burhan Mohamed ambaye ni mwa viongozi wa Lions Club nchini Tanzania 

Aliyesimama ni afisa elimu msingi katika manispaa ya Shinyanga bi Pudensiana Kihawa alizungumza katika shule ya msingi Town ambapo alikipongeza chama hicho kwa kutoa msaada wa madawati katika shule hiyo na kupongeza jihitada za meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam kwa kutafuta wafadhili hao

Tunafuatilia kinachoendelea..... 

Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam ,ambaye ni diwani wa kata ya Shinyanga mjini,akizungumza katika shule ya msingi Town ambapo alisema amekuwa akishirikiana na Lions Club katika mambo mbalimbali na aliwaomba msaada wa madawati hawakusita kumpatia 

Meya huyo alisema Lions Club wamekuwa wakitoa misaada mbalimbali katika mkoa wa Shinyanga na hivi karibuni walitoa msaada wa chakula kwa waathirika wa Mvua ya mawe katika Kata ya Mwakata wilayani Kahama sambamba na kutoa msaada wa chakula kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga zote hizo zikiwa ni juhudi zake kusaidia wananchi kupitia wafadhili mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania 

Mwenyekiti wa Lions Club kanda ya ziwa bwana Lion Parimal Patel akizungumza wakati wa kukabidhi madawati hayo ambapo alisema chama chake kinalenga kusaidia jamii zaidi 

Bwana Lion Burhan Mohamed ambaye ni mwa viongozi wa Lions Club akizungumza katika shule ya msingi Town 

Mwenyekiti wa Lions Club International katika nchi ya Uganda na Tanzania bwana Lion Patel Yogesh akizungumza katika shule ya msingi Town ambapo alitoa wito kwa wazazi kupeleka watoto wao shule na kuahidi kutoa madawati mengine 164 na kupaka rangi majengo ya shule hiyo kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu 

Mwenyekiti wa Lions Club International katika nchi ya Uganda na Tanzania bwana Lion Patel Yogesh akisisitiza jambo

Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam akikabidhi Laptop kwa diwani wa kata ya Kizumbi na mwalimu wa shule ya Sekondari Kizumbi iliyotolewa na Lions Club kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya kitaaluma katika shule hiyo 

Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam akishikana mkono na diwani wa kata ya Old Shinyanga na mwalimu wa shule ya sekondari Old Shinyanga wakati wa kuwakabidhi laptop 

Afisa mtendaji wa kata ya Shinyanga mjini na walimu wa Town Sekondari wakishikana mkono na meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh wakati wa kupokea laptop 
Mwenyekiti wa Lions Club International katika nchi ya Uganda na Tanzania bwana Lion Patel Yogesh akikata utepe wakati wa zoezi la kukabidhi madawati 100 

Meya na viongozi wa Lions club wakiwa wamekaa kwenye madawati hayo 

Katibu wa Lions Club mkoa wa Shinyanga bwana Lion Sandip Lakhani akizungumza wakati wa kukabidhi madawati hayo 100

 
Baadhi ya wazazi wakiwa eneo la tukio 

Baadhi ya wazazi na walimu wakiwa eneo la tukio,wakiwa wamekaa kwenye madawati yaliyotolewa na Lions Club 

Muonekano wa karibu wa madawati hayo ya chuma 

Baadhi ya madawati hayo yakiwa shuleni 

Hapa ni katika Kituo cha walemavu wa ngozi cha Buhangija mjini Shinyanga.

Chama cha Kimataifa Lions Club International pia kimetoa msaada chakula katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa Ngozi cha Buhangija ili kuwapunguzia changamoto kubwa ya chakula. 

Lions Club imetoa kilo 50 za mchele,kilo 100 za unga wa ugali,mafuta lita 20,sabuni boksi moja na boksi 2 za biskuti kwa ajili ya watoto hao,ambapo sasa kuna wenye albinism 301,wasioona 40 na wasiosikia 64. 

Kushoto ni mwenyekiti wa Lions Club International katika nchi ya Uganda na Tanzania bwana Lion Patel Yogesh,kulia ni meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam wakiwa katika kituo cha Buhangija leo Jumapili Julai 05,2015 

Aliyesimama ni kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Josephine Mabula akizungumza katika kituo cha Buhangija ambapo alisema watoto hao wameshafanyia utaratibu wataanza kupatiwa ruzuku kutoka serikalini na utaratibu mwingine unaoendelea hivi sasa ni kutafuta eneo kwa ajili ya kuwajengea mabweni kupitia wafadhili mbalimbali

 
Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam akizungumza katika kituo cha Buhangija

Viongozi mbalimbali wa Lions Club wakiwa katika kituo cha Buhangija leo 

Mwenyekiti wa Lions Club International katika nchi ya Uganda na Tanzania bwana Lion Patel Yogesh akizungumza katika kituo cha Buhangija ambapo alisema wanajipanga kuleta msaada mwingine mkubwa zaidi kwa watoto hao

Kulia ni Mkuu wa kituo cha Buhangija mwalimu Peter Ajali akipokea chakula kutoka Lions Club 

Mwenyekiti wa Lions Club Shinyanga bwana Jayantizal Pattani akikabidhi boksi la sabuni 

Zoezi la kukabidhi misaada linaendelea 

Mwalimu Peter Ajali akipokea mafuta ya kupikia 

Mwalimu Peter Ajali akiweka sawa ndoo ya mafuta ya kupikia

Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog Shinyanga 


0 maoni:

Post a Comment