Mwenyekiti wa Kampeni iliyolenga kupata fedha kwa ajili ya kuwasaidia wanahabari
wanaougua magonjwa sugu yakiwepo ya saratani, (MEDIA CAR WASH FOR CANCER)
, Benjamin Thompson akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza kiasi
cha fedha kilichopatikana katika harambee ya jijini Dar es Salaam ambapo kiasi cha
shilingi Milioni 31 zilipatikan ikiwa ni ahadi na taslimu. Kulia ni Mjumbe wa Kamati hiyo
ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi wa MAELEZO, Zamaradi Kawawa. Harambee
nyingine kama hiyo inataraji kufanyika Jijini Mwanza mwezi Agosti mwaka huu.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Dar es Salaam Julai 9, 2015
JUMLA ya shilingi milioni 31 zimepatikana katika harambee ya kuosha magari iliyofanywa na waandishi wa habari Julai 4, 2015 katika viwanja vya Leaders Club, Jijini Dar es Salaam. Kati ya fedha hizo, taslimu ni Milioni 12 na zingine ni ahadi.
Harambee hiyo inajulikana kwa jina la Media Car Wash for Cancer. Lengo la changizo hilo lilikuwa kupata Shilinngi Milioni 100, ili kuwahudumia waandishi wenye matatizo mbalimbali ya kiafya pamoja na kuwaingiza waandishi wa habari kwenye mfumo rasmi Bima ya Afya.
Kama tulivyotanzaga awali, wagonjwa ambao ni walengwa Adolf Simon Kivamo, Dastan Bahai na Athumani Hamisi.
Ili kutimiza lengo la changizo, Kamati ya Media Car Wash for Cancer inatarajia kuendelea na zoezi la kutafuta pesa mpaka kiwango hicho kitakapofanikiwa.
Mpaka sasa Kamati imeweza kuunda kamati ndogondogo zitakazosimamia zoezi la ufuatiliaji na ukusanyaji fedha kulingana na ahadi mbalimbali na wataifanya kazi hiyo kwa muda wa wiki moja.
Kisha, wajumbe wa kamati hii ambayo jumla yao ni 75 watatoa maamuzi wa mgao huo mara moja.
Kamati hizo pia zitafanya kazi ya kuwatambua idadi ya kamili ya waandishi wengine wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali na hawana msaada unaoeleweka.
Aidha, hali kadhalika, kamati hiyo pia inafanya tathimini ili kujua idadi ya wanahabari ambao hawana Bima ya Afya ili utaratibu wa kuwaingiza kwenye mpango huo uandaliwe.
Katika awamu hii ya kwanza tunatarajia kuanza na wanahabari 50 ambao sio waajiriwa, lakini wanafanya kazi katika vyombo vya habari nchini yaani correspondents.
Uteuzi wa majina ya waandishi utakwenda kwa kufuatana, yaani kutoka na chombo kimoja hadi kingine.
Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Tanzania kwa waandishi wa Habari kuwa na mfuko huu ambao lengo lake ni kwasaidia katika masuala ya matibabu.
Kamati itaanza na waandishi wa habari walioko kwenye vyombo vya habari vya Jijini Dar es Salaam na baadaye kuendelea katika mikoa mingine nchini.
Aidha, Kamati ya Maandalizi ya Harambee hii imeitisha mkutano mkuu wa wadau wa habari nchini utakaofanyika alhamisi Julai 16, 2015 kwa ajili ya kuanzisha mchakato wa usajili wa chombo hiki muhimu.
Wahariri wenu watakujulisheni muda na mahali utakapofanyika mkutano huu.
Pia, kamati hii inakusudia kufanya harambee nyingine katikati ya mwezi Agosti mwaka huu, itakayofanyika Jijini Mwanza.
Hatua za awali za harambee hiyo kwa kushirikiana na wenzetu wa Jiji hilo zimeanza,ikiwa ni pamoja na kutafuta eneo la kufanyia shughuli hiyo pamoja na wadhamini mbalimbali.
Mwisho tungependa kutoa shukrani zetu za dhati kwa wadhamini na wadau wote walioshirikiana nasi katika harambee hii ambao ni BOT,TPB, NHIF, TANAPA, NSSF, JUBILEE INSURANCE, ANSAF, ASTE INSURANCE, MOIL,TAGCO,TEA, Wizara Ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,Bw. Reginald Mengi, Mh.Hamis Kagasheki, Mh. Ridhiwani kikwete, Mh.Shabiby, Clouds FM, Radio Five,New Habari. The Guardian Ltd, pamoja na Wanakamati,
Benjamin Andongolile Thompson
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi
Media Campaign for Cancer Campaign
0 maoni:
Post a Comment