Na Yohana
Mfanyabiashara wa duka la vipuri vya magari mjini Tarime mkoani Mara, Tumaini Jacob amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya akituhumiwa mauaji ya askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Anadaiwa kumuua askari huyo wa Kikosi cha Nyandoto, Roja Elias kwa kumpiga risasi tumboni wakati wakiwa baa moja mjini hapa baada ya kutokea ugomvi wa kunyang’anyana mwanamke ambaye ni mhudumu wa baa hiyo.
Alisomewa mashitaka hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Tarime, Marther Mpaze.
Mwendesha Mashitaka wa Polisi, George Lutonja alidai kuwa Jacob (45) Agosti 17 usiku saa 6 .30 wakati akiwa baa na Hoteli ya NK, kulitokea ugomvi kati yake na askari huyo.
Alidai katika ugomvi huo, Tumaini alichomoa bastola yake na kumpiga risasi Roja tumboni na kutokea mgongoni.
Majeruhi huyo alikimbizwa Hospitali ya Wilaya ambapo hali yake ilizidi kuwa mbaya na kuhamishiwa Hospitali ya Rufaa Bugando ambapo mauti yalimkuta akipatiwa matibabu katika hospitali hiyo ya Bugando Mwanza.
Mtuhumiwa huyo Tumaini hakutakiwa kujibu lolote, kwani mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji
0 maoni:
Post a Comment