Tayari mtandao huo wa kijamii wa
Facebook unakusanya taarifa kutoka katika picha zako ili kubaini migao ya maoni
kutoka kwa marafiki wako pale wanapoweka mtandaoni picha.
Sasa
inaonekana mitandao ya kijamii inachukua mkondo mwingine wa kuboreshwa zaidi.
Watafiti kutoka katika idara ya upelelezi ya Facebook wamekuwa
wakiifanyia kazi teknolojia hiyo mpya ambayo nia kuu ni kumtambua mtu hata kama
uso wake hauonekani bayana kwenye picha.
Teknolojia hiyo iitwayo 'algorithm', inaangazia zaidi ya viungo
mia moja vya mwanadamu.
Inatumika kwa pamoja katika kutambua uso wa mtu na pia mwili
mzima wa binadamu.
Watafiti hao walitumia njia hiyo kwa kuzifanyia majaribio picha
elfu 37 za watu ambazo zilitolewa kutoka kwa 'Flickr Commons'.
Wanasema kuwa njia hiyo ilitoa matokeo asilimia 83 ya watu 581
tofauti.
Matokeo hayo yaliwasilishwa mapema mwezi huu wa Juni katika
kongamano la wakfu wa Computer Vision.
0 maoni:
Post a Comment