HILI NDILO DARAJA LA MITI LILILOPO MKOANI SIMIYU..



Hili ni Daraja la miti katika Mto Duma uliopo katika Kijiji cha Gibishi wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, ambalo limetumika kwa muda wa miaka 20 na wananchi wa vijiji vya Gibishi na Mwauchumu vinavyotenganishwa na daraja hilo.




 

Muonekano wa daraji hilo

Daraja la Miti

Daraja jipya la kisasa katika mto Duma ambalo limejengwa na serikali.
 ************
Baada ya kuteseka kwa zaidi ya miaka 20 kuvuka mto Duma uliopo katika kijiji cha Gibishi wakazi wa vijiji vya Gibishi kata ya Gibishi na Mwauchumu kaya ya Girya katika halmashauri ya wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, hatimaye wametatuliwa kero hiyo kwa kujengewa daraja la kisasa.
Wakazi hao ambao ni zaidi 7450 wamekuwa wakiteseka kuvuka mto huo hasa kipindi cha mvua kutokana na kukosa daraja kwa kulazimika kutumia daraja la miti  lililokuwa likihatarisha maisha yao wakati wa kuvuka kutokana na kutokuwa imara.

Wakiongea mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Juma Chum wakati mwenge wa uhuru ulipofika katika vijiji hivyo kuzindua daraja mbadala,wananchi  walisema wamekuwa wakikosa huduma muhimu za kijamii kutokana na kuwepo kwa mto huo mkubwa.

Walieleza kwa muda wa miaka 20 wagonjwa wamekuwa wakifia katika mto huo kutokana na kushindwa kuvuka kwenda katika kijiji kingine kufuata huduma ya afya hasa kipindi cha masika, sambamba na kukosa huduma nyingine za kijamii.
“wakazi hao walisema mbali na wagonjwa hao kupoteza maisha wakati wa kuvuka mto huo, pia hata wakazi wa hao ambao si wagonjwa, watoto, na wazee wamekuwa wakitumbukia ndani ya  mto huo na kupoteza maisha pindi wanapovuka kutafuta huduma nyingine katika maisha yao",Alisema Mwasi Juma mkazi wa Gilya.

Mto huo unaotenganisha vijiji hivyo ulielezwa na wananchi hao kuwa kikwazo kikubwa katika kujiletea maendeleo, huku wakiishukuru serikali kwa kuwatatulia kero hiyo baada ya kujengwa daraja lililo imara.

“ Tunaishukuru serikali kwa kutatua kero hii….tumeteseka sana tangu nimezaliwa hapa wakati wa kipindi cha masika ni tabu, wengine wameishapoteza maisha kutokana na mto huu….kuna daraja la miti tulitengeneza sisi wananchi lakini haliko imara” ,alisema Magembe Shagi

Akisoma taarifa ya ujenzi wa daraja hilo mbele kiongozi huyo wa Mwenge taifa Mhandisi wa halmashauri hiyo Alexander Matoyo alisema jumla kiasi shilingi 459,453,650 zimetumika kujenga daraja hilo ambazo ni fedha kutoka serikali kupitia mfuko wa barabara.

Matoyo alieleza kuwa ujenzi wa mradi huo ulianza kutekelezwa mweze Juni mwaka 2014 ambapo utengezaji wakeulikamilika   Juni mwaka huu chini ya Mkandarasi VIRGIN CIVIL LTD.

Akiongea na mamia ya wananchi waliofika eneo hilo mara baada ya kufungua daraja hilo Kiongozi huyo alisema kuwa dhamira ya serikali ni kuhakikisha watanzania wote wanaeletewa maendeleo kwa kuletewa huduma za kijamii na kiuchumi karibu na maeneo yao.

Aidha aliwataka wananchi hao kutunza daraja hilo ili lidumu kwa muda mrefu hasa kwa kuhakikisha miundombinu yake inalindwa ili isiibiwe na baadhi ya watu.

“ Kila mmoja awe mlinzi wa mwingine kuhakikisha miundombinu ya daraja hili inalindwa…..fedha nyingi za serikali zimetumika katika kukamilisha ujenzi huu…na hii imeonekana kuwa kero kubwa kwenu na sasa imetatuliwa kwa kiasi kikubwa kikubwa na kutunza” Alisema Chum.

0 maoni:

Post a Comment