MBOWE ASEMA ALIKO DR.SLAA ATAJA ALIKO NA KWANINI HAONEKANIM KWENYE VIKAO..

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akihojiwa na kituo kimoja cha Radio amesema Katibu wa Chama hicho ni mzima, yuko kwenye likizo ya wiki moja, wanachama wasiwe na hofu.

Akizungumza na Radio one mda huu saa 4, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) Freeman Mbowe, amesema Dr Slaa hawezi kuhama chama hicho na hafikirii kamwe, kwa sasa anapumzika kwa likizo ya wiki moja. 

Alipoulizwa kuhusu Slaa kutokubaliana na ujio Wa Lowassa amejibu kila kitu tulikubaliana na Slaa mwenyewe aliunga mkono suala hilo.

Mbowe amesema wananchi na wanachadema kwa ujumla wasiwe na wasiwasi kwani hiki chama ni makini na hakiwezi fanya maamuzi bila maridhiano na akasisitiza kuwapuuza wanaoeneza habari kuwa Slaa amejiuzulu siasa.

Alipoulizwa mara ya mwisho kuwasiliana na Dr Slaa ni lini akajibu jana saa kumi na mbili jioni.

Alipoulizwa walizungumza nini akajibu anajua yeye na Slaa.

Walipomuuliza hasa mbona sisi tukimpigia hapatikani akajibu sijui lakini mimi nimewasiliana nae jana.

0 maoni:

Post a Comment