NA HILI NI AGIZO LA WAZIRI MKUU KWA JESHI LA MAGEREZA KUTIMIZA..!!!




Waziri mkuu Mhe.Mizengo Pinda ameliagiza jeshi la magereza nchini kutumia rasilimali kubwa waliyonayo ya ardhi na watu kuongeza uzalishaji wa chakula kwa ajili ya mahitaji ya jeshi hilo na ziada kutumika kusaidia majeshi mengine nchini badala ya kuendelea kutegemea bajeti ya serikali.


Akifunga mafunzo ya uongozi daraja la kwanza, kozi ya 21 ya askari wa jeshi la magereza, katika chuo cha magereza kiwira wilayani Rungwe, waziri mkuu Mhe. Mizengo Pinda amelitaka jeshi hilo kutumia rasilimali kubwa ya ardhi pamoja na watu walionao kuongeza uzalishaji wa chakula kwa ajili ya matumizi ya jeshi hilo na ziada isaidie majeshi mengine nchini.

Mkuu wa jeshi la magereza nchini, kamishna jenerali wa magereza, John Minja amesema kuwa jeshi hilo limekamilisha na kuwasilisha serikalini sera mpya ya jeshi la magereza ambayo ikipitishwa itawezesha jeshi hilo kuwa na mwelekeo mpya, huku katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi, Mbarak Abduwakil akimwomba waziri mkuu kutumia muda wake mfupi uliosalia kuipitisha sera hiyo.

Kwa upande wake mkuu wa chuo cha magereza kiwira, kamishna msaidizi wa jeshi la magereza Stanford Ntilidura amesema kuwa mafunzo waliyoyapata askari hao ni ya kiwango cha juu na kupendekeza kuwa wahitimu wote watunukiwe cheo cha coplo.

0 maoni:

Post a Comment