Via Bongo5 Blog
Bazara la Sanaa Taifa (BASATA) limeeleza ni wasanii gani ambao ni lazima kujisajili na ambao sio lazima kujisajili na baraza hilo ili kupata kibali cha kufanya shughuli za sanaa.
Akiongea katika semina ya wasanii wanaowania tuzo za EATV Award Jumatano hii, Mtafiti wa shughuli za sanaa kutoka Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Bwana Selemani ameainisha ni aina gani ya wasanii ambao wanaweza kufanya shughuli za sanaa bila kujisajili.
“Jukumu la baraza ni kuwasajili na kuwatambua wasanii wa muziki, filamu au kundi kwa kutoa vibali vya kufanya shughuli za sanaa, hata kama ni watu sio lazima msanii ambao wanashiriki kwenye sanaa kibiashara au una shiriki kwa kupata faida ni lazima kujisajili ili uweze kutambuliwa na baraza na kupatiwa vibali vya kufanya shughuli ya sanaa,” alisema Seleman.
Aliongeza, “Lakini kama unafanya sio kwa ajili ya kupata faida sio lazima kujisajili au kama unafanya pasipo kuwa na mtazamo wa kibiashara basi kwako suala la kujisajili nila hiyari,”
0 maoni:
Post a Comment