Jackie Chan atunukiwa tuzo ya heshima ya Oscar

Baada ya kuigiza filamu takriban 200, hatimaye Jackie Chan ametunukiwa tuzo ya heshima ya Oscar.
1479044482057
Muigizaji huyo wa China alipewa tuzo hiyo Jumamosi kwenye tuzo za Governors.
“After 56 years in the film industry, making more than 200 films, after so many bones, finally,” alisema Chan, 62.
Muigizaji huyo alikumbushia kuwa kuna wakati alikuwa akiangalia tuzo hizo na wazazi wake ambapo baba yake alimuuliza iweje hajawahi kushinda Oscar licha ya kuwa na filamu kibao.
“I continue to make movies, jumping through windows, kicking and punching, breaking my bones,” alisema.
Muigizaji huyo alitambulishwa na staa mwenzake wa filamu ya “Rush Hour” Chris Tucker, muigizaji Michelle Yeoh na Tom Hanks, ambaye alimuelezea kama “Jackie ‘Chantastic’ Chan.”
Hanks alisema kuwa ni jambo zuri kutambua kazi za Chan kwa sababu filamu za martial arts na action comedy, zimekuwa zikitengwa kwenye tuzo.
Muigizaji mkongwe, Arnold Schwarzenegger amempongeza Chan kwa tuzo hiyo.
15099460_341490366213624_1734472102393675776_n
Kwenye picha hiyo juu aliyoiweka Instagram, Schwarzenegger ameandika: Congratulations to my great friend Jackie Chan on his fantastic honor – after 200 movies, you certainly deserve this Oscar. You always inspire.

na Yohana Blacklista

0 maoni:

Post a Comment