Sababu ya kuanguka kwa ndege iliyobeba wachezaji wa Chapecoense yatajwa

Sababu iliyosababisha kuanguka kwa ndege iliyowabeba wachezaji wa timu ya Chapecoense ya nchini Brazil imetajwa.
crash-site-colombia_foreign_1-large_transdededsifil4jmjaxpgpd5kxqkm4rklcappyq5xdlz-a
Kwa mujibu wa taarifa za ndani kutoka kwenye kifaa cha kurekodia mawasiliano imedaiwa kuwa ndege hiyo iliishiwa mafuta.
Katika hatua nyingine kutoka kwenye mnara wa mawasiliano ya ndege, rubani alisikika akirudia mara kadhaa akiomba ruhusa ya kutua kwa dharura kutokana na hitilafu ya umeme iliyokuwamo ndegeni pamoja na kuishiwa mafuta ya ndege.
Wakati huo huo jeshi la nchi ya Colombia limeliambia shirika la habari la AFP kuwa pamoja na ndege hiyo kuanguka kuna shaka juu ya ajali hiyo kwani pamoja na ndege hiyo kuanguka hakukuwa na mlipuko wowote na kwamba huenda kulitumika nguvu nyingine tofauti na nadharia ya kwisha kwa mafuta ndegeni.
Hata hivyo wadadisi wa mambo na wachunguzi bado hawako tayari kufungua mdomo na kuzungumzia juu ya chanzo chochote cha ajali hiyo na kwamba taarifa kamili ya uchunguzi itatolewa baada ya miezi kadhaa.

0 maoni:

Post a Comment