Pep Guardiola akaribia kustaafu kufundisha soka

Kocha wa klabu ya soka ya Manchester City, Pep Guardiola amefunguka kuwa umri wake wa kustaafu kufundisha soka umekaribia.
Guardiola ambaye alisaini mkataba wa miaka mitatu wa kuifundisha City kuanzia msimu huu, ameiambia NBC Sports kuwa hataweza kufundisha soka kwa muda mrefu tofauti na mwanzoni alivyowahi kusema kuwa atastaafu kufundisha mchezo huo pindi atakapoofika umri wa miaka 60 au 65.
“I will be at Manchester for the next three seasons, maybe more, but I am arriving at the end of my coaching career, of this I am sure. I will not be on the bench until I am 60 or 65 years old. I feel that the process of my goodbye has already started,” amesema Guardiola.
Kwa sasa kocha huyo ana umri wa miaka 45 na hutakiwi kushangaa Man City ndio ikawa timu yake ya mwisho kuifundisha kwa kuwa ameshafanikiwa kuchukuwa vikombe vyote vikubwa duniani kwenye ngazi za vilabu huku akifanikiwa kuzifundisha timu kubwa kama Barcelona, Bayern Munich na sasa Man City.

0 maoni:

Post a Comment