Rama Dee adai angekuwa Rais wa Tanzania angewekeza kwa watoto

Msanii wa muziki Rama Dee amedai kama angekuwa Rais wa Tanzania angeanza kuwekeza kwa watoto kwa kuwa watoto ndiyo taifa la kesho.

Rama Dee akiwa na mafilia yake
Hatua hiyo imekuja baada ya rapper Nikki wa Pili kusikitishwa na jinsi watoto wadogo wanavyotumia vibaya mitandao ya kijamii.
“Unapotizama vijana wa miaka 16-24 mtaani na mtandaoni, utagunduwa hakuna uongozi mgumu duniani kama kuwa mzazi,” alitweet Nikki wa Pili.
Kauli hiyo ilifanya Rama Dee kufunguka mambo mengi kuhusu malezi ya watoto na kudai kuwa kama yeye angekuwa Rais wa Tanzania angewekeza kwa watoto kwa kuwa ni kizazi cha kesho.
Muimbaji huyo aliandika
Nikki ameongea kitu kizuri sana hapa! Ila kwa kuongezea tu,Wazazi wengi sana wanaishi kwa msongo wa mawazo kutokana na Watoto wao kwenda Nje ya misingi waitakayo au dreams zao.
Lakini kuna kitu kinaitwa Uhuru wa kuishi na kufikiri pia, Wazazi wengi wanasahau kuwa Mtoto ana haki ya kusikilizwa pia, na mtoto akili yake inakuwa kubwa kila siku, na kuna muda ikiwa kubwa zaidi baadhi yao wanaishusha bila kuelewa!
Kuna baadhi ya misemo ni sumu kuyatamka Kama Mzazi.
1)Anajifanya anajua
2)Lione
3)Mbwa wee
4)Hauwezi kufanikiwa
5)Ndugu zako hawajasoma utasoma wewe..
6) Hauwezi
7) Hapana “NO” bila sababu
Misemo mingi sana inaweza mfanya Mtoto asijiamini na kuona yeye wa kusaidiwa tu!
Kwa mfano mimi nigekuwa Rais wa Tanzania 🇹🇿 ninge wekeza kwa watoto mana hauwezi kuinyoosha Nchi bila kuangalia kizazi cha kesho, hiki chetu tayari kimeathirika!🎅🏿
Kwa mfano nchi Ya Australia iligundua Stress nyingi sana za wazazi zinaaribu maisha ya Watoto, so walicho kifanya walitengeneza sheria ya Mtoto, Na Kama mzazi ukipindisha unapelekwa mahakani bila shaka. Waliweza kutengeneza Mfumo wa “childcare” so hata Kama mzazi hana kipato lakini serikali inaweza kusaidia Mtoto akapata Msingi Mzuri Wa kimaisha na kishule! Child care Wanajaribu kusaidia wazazi wafanye kazi na Mtoto apate malezi Mazuri kupitia Watu walio na uzoefu wa kulea Watoto! Ndio maana ukimsimamisha mtoto wa Masikini wa mzungu na tajiri wote wapo sehemu Sawa tu! So dhumuni la serikali hapa ni kukamilisha au kutimiza dreams za watoto!
Watoto huzaliwa na Akili na jinsi ya kuiboresha au kuikomaza au kwa lugha nyepesi kumfanya mtoto awe bora, wala sio gharama ni bure kabisa!
Tumia neno, Good boy—>Mtoto mzuri kila akifanya jambo ambalo ni sahihi
2) Tumia kumuelimisha pindi usemapo “NO” au hapana, kwa sababu ndani ya akili ya watoto kuna kitu “Why” katika kila jambo ulisemalo
Attentions….hili ni muhimu kuliko yooote!
Nipo na mambo mengi ya kuandika next time tutaendele kujadili. Rama Dee

0 maoni:

Post a Comment