Wenger afunguka kuhusu mipango yake ya usajili dirisha dogo

Kocha Arsene Wenger baada ya kupata ushindi wa mechi mbili mfululizo amedai kuwa anafurahia ubora wa kikosi chake cha Arsenal na kwa sasa hana mpango wa kuleta wachezaji wapya dirisha la uhamisho Januari.
Gunners wamerejesha kiwango chao bora cha msimu kwa mara nyingine baada ya wiki iliyopita kupata ushindi na kukwea hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi huku wakiwa nyuma ya vinara Chelsea kwa tofauti ya pointi tisa.
Arsenal wamekuwa wakikuvutiwa na wachezaji wengi tangu majira ya joto, ikiwa ni pamoja na Ross Barkley, Julian Brandt na Franck Kessie, lakini Wenger hatarajii kufanya usajili wowote majira ya baridi na badala yake atajitahidi kuwanoa wafungaji wake wawe katika kasi ya juu zaidi.
“Hakuna mpango wowote kwa sasa,” aliiyambia BBC Sport baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Crystal Palace Jumapili usiku. “Unaweza kuangalia wachezaji tuliowakosa leo hakuna Santi Cazorla na Mesut Ozil, tunatumaini kuwa nao tena mechi ijayo. Danny Welbeck anarejea, na tuna kikosi kikubwa.” alisema Wenger
Arsenal sasahivi bado wapo kwenye mazungumzo na wachezaji wao Mesut Ozil na Alexis Sanchez, ambao wote wana muda usiozidi miezi 18 kwenye mikataba yao ya sasa.

0 maoni:

Post a Comment