Naibu waziri wa Nishati na Madini nchini Tanzania
mheshimiwa Stephen Masele ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini
mkoani Shinyanga amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuvamiwa na watu
wanaosadikiwa kuwa ni vibaka na kumpora Wallet na kadi 6 za benki usiku wa
kuamkia leo ikiwa ni saa chache tu zikiwa zimesalia kuanza kufanyika kwa
uchaguzi wa serikali za mitaa kote nchini leo Jumapili Desemba 14,2014.
Akizungumza hivi punde Masele amesema tukio hilo limetokea
jana usiku majira ya saa 4 usiku wakati akishuka kwenye gari lake ili kuingia
katika zahanati ya Majengo mjini Shinyanga kwa ajili yakupata matibabu kwani
alikuwa anajisikia kuumwa baada ya kampeni za uchaguzi kumalizika.
"Ghafla nilivamia na watu na kundi la watu wanaodhaniwa kuwa ni
vibaka,walinidhibiti katikati ya mlango wa zahanati na kunipora simu yangu ya
mkononi yenye line ya Voda na Tigo,pochi yangu ya kuhifadhia pesa,lakini
nawashukuru askari wa jeshi la polisi waliokuwa doria kwa kufika haraka eneo
la tukio na kunipa msaada",aliiambia Malunde1 blog.
"Naomba wananchi wawe watulivu wakati polisi wakiendelea na
uchunguzi",aliongeza Mheshimiwa Masele.
Hata hivyo kuna taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba
mheshimiwa Masele alifanyiwa vurugu wakati akitoa rushwa kwa wananchi
|
0 maoni:
Post a Comment