Watu kadhaa wanashikiliwa
mateka na mtu mmoja au zaidi wenye silaja katika mgahawa wa Lindt mjini Sydney,
Australia.
Mamia ya Polisi
waliojihami kwa silaha wamezingira eneo lilipotokea tukio hilo.
Takriban watu watatu
wameonekana ndani ya mgahawa wakiwa wamenyanyua mikono juu wakiwa wameiegesha
kwenye dirisha wakiwa wameshika bendera nyeusi ikiwa na maandishi ya kiarabu.
Waziri Mkuu wa Australia
Tony Abbot amesema tuki hilo linahuzunisha sana.
Abbot amesema
haijajulikana nani alihusika na tukio hilo hata hivyo anahisi huenda ni njama
za kisiasa na kuwa tayarikamati ya usalama ya taifa imepewa taarifa.
Kamishna wa Polisi wa
South Wales Andrew Scipione amesema tukio hilo halichukuliwi kuwa la kigaidi
lakini imethibitishwa kuwa kuna mtu mwenye silaha anayewashikilia mateka watu
kadhaa.
Mashahidi wa tukio hilo
wamesema walimuona mtu akiwa na begi na silaha akiingia kwenye mgahawa, polisi
wamefunga eneo hilo, barabara na kuwaondoa watu katika eneo hilo.
na Yohana Emmanuel
0 maoni:
Post a Comment