Mwenyekiti wa BAVICHA taifa Patrobas Katambi
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(BAVICHA) taifa Patrobas Katambi ametangaza kuwania ubunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia UKAWA katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Katambi ametangaza nia hiyo jana jioni wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mahakama ya Mwanzo Nguzo nane Mjini Shinyanga,mkutano ambao umehudhuriwa na mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema.
Akizungumza katika mkutano huo mwenyekiti wa BAVICHA Katambi alisema yeye ni mzaliwa wa Shinyanga hivyo atakomaa katika jimbo la Shinyanga Mjini kuhakikisha anagombea ubunge ili kuondoa uongozi wa Chama Cha Mapinduzi ambao umekuwa ukifanya ubadhirifu wa fedha na kutowaletea maendeleo wananchi.
“Mimi ni mtu wa Shinyanga,Natangaza rasmi kuwa nitagombea ubunge katika jimbo la Shinyanga Mjini,uwezo ninao na nia ninayo,naungana na watangaza nia wengine waliotangulia,naomba ushirikiano tu,kama jina langu litapitishwa tutafanya mambo makubwa katika jimbo hili”,alieleza Katambi.
Alisema endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo nitakuwa mbunge wa Vitendo siyo maneno kama wanavyofanya wabunge wa CCM hasa katika jimbo la Shinyanga ambao kazi yao ni kuongea tu na kula pesa za jimbo ba kuwaacha wananchi wakiendelea kuwa maskini kila kukicha.
|
0 maoni:
Post a Comment