|
|
Watangazaji
veronica natalis,richard ndariro,dj hunter na msanii wa bongo movie
shinyanga aliyefukuzwa uanachama amina francis mwandu
|
|
Richard ndariro,dj hunter,veronica natalis na amina mwandu
|
Kumekuwepo na sintofahamu
baina ya wasanii katika kundi la wasanii wa kuigiza “bongo movie shinyanga”,ambapo baadhi
ya wasanii wa kundi hilo wakimtupia lawama mwenyekiti wa bongo movie shinyanga.
Inaelezwa kuwa
kinachoendelea hivi sasa ni kwamba mwenyekiti wa bongo movie shinyanga juma
ibrahimu songoro "songoro
gaddafi" anashikiliwa na jeshi la polisi shinyanga kwa kosa la
kumtishia kumuua aliyekuwa katibu wa bongo movie shinyanga sophia kichochi
baada ya kudai mshahara wake kutokana na kufanya kazi kwa muda mrefu bila kulipwa.
Miongoni mwa wasanii wa
kundi hilo amina francis mwandu anasema migogoro imeanza mwezi machi mwaka huu
baada ya filamu ya firigisi kumaliza kurekodiwa ambapo mwenyekiti alimfukuza
katibu wake akidai kuwa anavujisha siri za ofisi baada ya hapo akamfukuza pia
msanii amina mwandu,mhusika mkuu katika filamu ya firigisi inayohusu mauaji ya
albino ambayo hata sokoni bado haijaingia.
Katika maelezo yake
songoro anasema alimfukuza katibu wake kutokana na utovu wa nidhamu huku
akikanusha kuwa siyo katibu wake bali alikuwa mfagiaji tu katika ofisi yao.
Hapa nimekurekodia
interview iliyofanyika kwenye kipindi cha faraja mamboleo kinachorushwa na
radio faraja fm ya shinyanga kila siku jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa tatu
asubuhi hadi saa saba mchana.
PICHA ZOTE NA Malunde1 Blog
0 maoni:
Post a Comment