KIKAO MAALUM CHA KUNUSURU SHIRECU SHINYANGA
Wajumbe wa kikao wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini |
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akitoa hotuba yake ambapo pamoja na mambo mengine aliitaka SHIRECU kuviendeleza vyama vya ushirika ambavyo vinasuasua ,huku akiwatahadharisha viongozi wa serikali na wanasiasa kuwa hawaruhusiwi kuwa viongozi ndani ya vyama vya ushirika ili kuepusha migongano ya kimaslahi.
Wakuu wa wilaya wakiwa ukumbini
Meneja mkuu wa SHIRECU mkoa wa Shinyanga Joseph Mihangwa akitoa taarifa ya shughuli za SHIRECU 1984 Limited ambapo alisema hadi kufikia Mwezi Machi 2015 ina vyama vya Ushirika vya Msingi wanachama hai 500 na vyama sinzia ( ambavyo havina kazi) 250
Mihangwa alisema katika msimu huu wa 2015/2016 wamejipanga kununua kilo milioni 15 za pamba katika mkoa wa Shinyanga,Simiyu na Geita kwani uwezo wa pesa upo.
Meza kuuu wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini |
Kikao kinaendelea |
Kikao kinaendelea ambapo wajumbe wa kikao hicho waliitaka Shirecu kuangalia uwezekano wa kuanza kuongeza thamani kwenye zao la pamba ili kupata faida zaidi na kuachana na mfumo wa kizamani wa kuuza pamba tu
0 maoni:
Post a Comment