UKAWA HATARI SANA MIKOANI NOMA SANA!!


**WAFANYA MAAJABU SHINYANGA MJINI!!!

**LEMA AFUNIKA!!!

**MGOMBEA WA UBUNGE APATIKANA!!!


Na MALUNDE1 BLOG
Hapa ni katika viwanja vya Mahakama ya Mwanzo Nguzo Nane mjini 

Shinyanga ambapo leo jioni mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema 

pamoja na mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chama Cha Demokrasia na 

Maendeleo (BAVICHA) taifa Patrobas Katambi wamehutubia maelfu ya 

wakazi wa Shinyanga na kutoa elimu ya uraia.Pamoja na mambo mengine 

Gobless Lema amewataka Watanzania kubadilika na kuacha tabia ya Uoga 

katika kufanya maamuzi magumu ikiwemo kuwaondoa madarakani viongozi 

wasio waadilifu...

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chama Cha Demokrasia na 

Maendeleo(BAVICHA) taifa Patrobas Katambi akizungumza katika mkutano 

huo ambapo alitangaza rasmi nia kugombea ubunge wa jimbo la Shinyanga 

Mjini Kupitia UKAWA katika uchaguzi mkuu mwaka huu.

Katambi alisema yeye ni mzaliwa wa Shinyanga hivyo atakomaa katika jimbo 

la Shinyanga Mjini kuhakikisha anagombea ubunge ili kuondoa uongozi wa 

Chama Cha Mapinduzi ambao umekuwa ukifanya ubadhirifu wa fedha na 

kutowaletea maendeleo wananchi.Baada ya kutangaza nia hiyo Umati wa 

watu ukapiga kelele nyingi wakiashiria kuwa walikuwa wanamsubiri kwa 

hamu atamke kuwa atagombea kwani anaonekana kuwafaa wakazi wa 

Shinyanga
“Mimi ni mtu wa Shinyanga,Natangaza rasmi kuwa nitagombea ubunge katika jimbo la Shinyanga Mjini,uwezo ninao na nia ninayo,naungana na watangaza nia wengine waliotangulia,naomba ushirikiano tu,kama jina langu litapitishwa tutafanya mambo makubwa katika jimbo hili, kwani najiamini na najua ninachokifanya,na siku zote mti wenye matunda ndiyo unaopigwa mawe,mimi naamini katika haki zaidi na kufuata sheria za nchi,mwaka huu lazima kieleweke”,alieleza Katambi.
Wakazi wa Shinyanga wakifuatilia kilichokuwa kinajiri eneo la

mkutano.
“Sijajipitisha kugombea,bali nitafuata taratibu za Chama

changu,nitaandika barua kupeleka jina langu ili kusimikwa kuwa mgombea

wa ubunge na endapo atapitishwa mtu mwingine zaidi yangu,tutamuunga

mkono kwani chama chetu ni cha Umoja na tunafanya kazi moja ya kuleta

ukombozi kwa wananchi”,alieleza  Katambi.

Kushoto ni Mtangaza nia ya Ubunge Shinyanga Mjini  Patrobas Katambi

akiwa na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema ambaye naye alijigamba

kuwania ubunge katika jimbo lake.

Wakazi wa Shinyanga wakifurahia baada ya kusikia kuwa Bwana Patrobas Katambi kuwa atawania ubunge katika jimbo la Shinyanga mjini ambalo sasa linaongozwa na mbunge wa CCM ndugu Stephen Masele
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema akizungumza na wakazi wa

Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine amewataka watanzania

Kumpuuza kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe kwa madai

 kuwa amepewa pesa na CCM ili azunguke nchi nzima kuvuruga

Chadema(UKAWA) lakini akasisitiza kuwa Kamwe Hataweza kwani

wameshajua anachokifanya ndiyo maana kwenye mikutano yake hathubutu

kuisema vibaya CHADEMA na maeneo aliyothubutu wananchi wamekuwa

wakimzomea.

Godbless Lema pia alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama nchini kufanya kazi

kwa kuzingatia sheria za nchi badala ya kupendelea chama Tawala.

Mbunge Lema pia alisema  Kitendo cha Zitto Kabwe kujitangaza kuwa ni

Mzalendo ni Unafiki Mtupu kwani Uzalendo haupimwi kwa Umaskini kwani

hakuna mtu anayependa kuwa maskini kila mtu anapenda kuwa na maisha

mazuri.

Mkutano unaendelea-Lema pia alidai kuwa Matatizo mengi yaliyopo nchini

Tanzania siyo CCM bali ni Uoga wa Watanzania wenyewe kufanya maamuzi

magumu


Jukwaa kuu wakifuatilia kilichokuwa kinajiri kwenye mkutano


Mkutano unaendelea

Jukwaa kuu wakifuatilia hotuba ya mheshimiwa Godbless Lema

Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la mkutano

0 maoni:

Post a Comment