|
Hapa ni katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi(Albino) wasiosikia na wasioona cha Buhangija Jumuishi kilichopo katika manispaa ya Shinyanga,ambapo leo Jumapili April 19,2015 Kkundi cha vijana kutoka Idara ya Vijana wa Kanisa la KKKT kanisa Kuu Ebenezer Shinyanga Mjini wametembelea kituo hicho kisha kuendesha maombi na baadaye kutoa msaada wa chakula na mahitaji mengine ya kibinadamu vyote vikiwa na thamani ya shilingi laki 6
Vijana hao wa KKKT kanisa Ebenezer Shinyanga Mjini wakiongozwa na mwenyekiti wao bwana Ombeni Kweka wametoa msaada wa mafuta ya kupikia ndoo 6,maharage kilo 50,mchele kilo 100,dawa za binadamu zenye thamani ya shilingi laki moja,pakti 4 za biskuti,kalamu 150,pipi,nguo na sabuni.Aliyesimama kulia ni mlezi/mkuu wa kituo cha Buhangija Peter Ajali akiwakaribisha vijana hao
Mwenyekiti wa kikundi cha Idara ya Vijana KKKT kanisa Kuu Enezener Ombeni Kweka akizungumza katika kituo cha Buhangija ambapo alisema vitendo vya ukatili wanaotendewa albino vinamuudhi mwenyezi mungu hivyo kuitaka serikali kuchukua hatua kali dhidi ya wahusika wa vitendo hivyo vya kikatili ikiwa ni pamoja na kuharakisha kesi zao ili vitendo hivyo visijirudie.
|
Mwenyekiti wa maombi idara ya Vijana wa KKKT kanisa kuu la Ebenezer Shinyanga mjini Astiye Mwaipopo akiongoza maombi maalum katika kituo cha Buhangija mjini Shinyanga.
|
Maombi yanaendelea-Kituo cha Buhangija hivi sasa kina watoto wenye ulemavu wa ngozi 284,wasioona 40 na wasiosikia 64 huku idadi ya albino ikiongezeka kila siku kutoka maeneo ya ndani na nje ya manispaa ya Shinyanga kwa hofu ya kuuawa.
|
|
Mwenyekiti wa maombi idara ya Vijana wa KKKT kanisa kuu la Ebenezer Shinyanga mjini Astiye Mwaipopo aliwataka watoto wenye ulemavu kutokata tama ili kutimiza ndoto zao kwani wapo watu wenye albinism wamefanikiwa katika maisha. |
|
Maombi yanaendelea-wa kwanza kushoto ni bwana Penny Nkya kutoka idara ya Vijana wa KKKT kanisa kuu Ebenezer Shinyanga mjini akifuatilia kwa ukaribu zaidi kilichokuwa kinaendelea
|
|
Katibu wa Vijana KKKT Ebenezer Kanisa Kuu Hoyce Mramu akinong’ona jambo na Mdeakonia wa kanisa la KKKT kanisa kuu Ebenezer Shinyanga Mjini Edna Shoo(wa kwanza kushoto) katika kituo cha Buhangija. |
|
Vijana wa KKKT kanisa kuuu Ebenezer Shinyanga mjini wakiwa Buhangija |
|
Katibu wa Vijana KKKT Ebenezer Kanisa Kuu Hoyce Mramu akionesha baadhi ya vitu walivyopelekwa kwa ajili ya watoto wenye ulemavu Buhangija |
|
Katibu wa Vijana KKKT Ebenezer Kanisa Kuu Hoyce Mramu akimkabidhi mtoto mwenye ulemavu wa ngozi boksi la Kalamu |
|
Katibu wa Vijana KKKT Ebenezer Kanisa Kuu Hoyce Mramu akishikana mkono na mtoto mwenye ulemavu wakati akikabidhi msaada kwa niaba ya wenzake. |
|
Makabidhiano yanaendelea-Mkuu wa kituo cha Buhangija Jumuishi Mwalimu Peter Ajali akizungumza wakati wa kupokea msaada kutoka kwa vijana wa KKKT ambapo pamoja na kuwashukuru kwa kuwafikia watoto hao pia hakusita kuiomba jamii kuendelea kukisaidia kituo hicho kinachokabiliwa na tatizo la Chakula,Vitanda,Magodoro,Masweta na dawa za binadamu.
|
|
Kijana Hassan Hamis akishukuru kupokea msaada kutoka kwa vijana wa kanisa la KKKT ,kwa niaba ya watoto wenye ulemavu katika kituo cha Buhangija. |
|
Hivi sasa kituo cha Buhangija kina watoto wenye ulemavu wa ngozi (albino) zaidi ya 280,wasiosikia 64 na wasioona 40,na idadi ya albino inaongezeka kila kukicha ambapo hadi April 19,2015 watoto albino wapo 284. |
|
Mkuu wa kituo cha Buhangija Peter Ajali akiwa amebeba mfuko wa pipi |
|
Mmoja wa vijana kutoka kanisa la KKKT akiwa amebeba mtoto katika kituo cha Buhangija |
|
Vijana wa kanisa la KKKT Ebenezer wakigawa pipi kwa watoto katika kituo cha Buhangija
|
0 maoni:
Post a Comment