ASKOFU WA TANZANIA AMTUNDIKA MIMBA MBILI MUIMBAJI WAKE WA KWAYA KANISANI !
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe mkoani Kagera, Benson Bagonza anayedaiwa kupiga mimba mbili nje ya ndoa na kutelekeza watoto.
Aibu! Peace Sylvester (36), mkazi wa Kijenge Juu jijini amefungua madai mazito kwenye Kituo Kikuu cha Polisi, Arusha kwa majadala mawili, AR/RB/4404/2015 KUTISHIA KUUA KWA MANENO na AR/RB/5290/2015 KUTELEKEZA FAMILIA dhidi ya Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Kagera, Benson Bagonza.
Peace alidai Askofu Bagonza ni mzazi mwenzake kwa kuzaa naye watoto wawili, Piana Bagonza (6) na Bariki Bagonza (3) lakini akadai amemtelekeza hivyo kuwa na maisha magumu katika kuwalea watoto hao.
AANIKA HISTORIA NDEFU
Peace alisema alianza kufahamiana na askofu huyo mwaka 2006 mjini Karagwe, Kagera akiwa ni muumini wa kanisa hilo akimtumikia Mungu kwa kuimba kwaya ya kanisa.
Alisema katika kuonana mara kwa mara na askofu huyo ndipo uhusiano ukaanza
lakini kwa makubaliano ya kutunza siri.
“Askofu aliniambia ana mke lakini ananipenda na anataka kuwa na uhusiano na mimi. Aliniahidi kunisaidia masuala mbalimbali iwapo nitamkubalia.
“Baada ya muda niliamua kumkubalia, tukawa na uhusiano na tulikuwa tunakutana mara kwa mara. Ilipofika mwaka 2008 nikapata ujauzito wa mtoto wa kwanza,” alisema Peace.
AHAMIA ILEMELA, MWANZA
Mwanamke huyo aliendelea kudai kuwa, baada ya kupata ujauzito, askofu huyo aliamua kumhamishia Ilemela mkoani Mwanza na kumpangishia chumba ambapo mwaka 2009 alijifungua mtoto wa kike, Piana.
AHAMIA ARUSHA
Peace aliendelea kudai: “Mtoto wangu alipofikisha umri wa miaka miwili, yaani mwaka 2010, askofu alinihamishia hapa Arusha na kunipangia chumba eneo la Kijenge Juu na kunitafutia kazi kwenye Hoteli ya Safari (New Safari Hotel). Hii hoteli inamilikiwa na KKKT.”
Watoto anaodaiwa kuwatelekeza |
Alisema: “Askofu alikuwa akija hapa Kijenge kumsalimia mtoto na kumwachia matumizi mbalimbali huku akisisitiza kutunza siri zaidi.”
ANASA MIMBA YA PILI
“Ilipofika mwaka 2011 nilipata ujauzito mwingine wa askofu ila cha kushangaza nilipomfahamisha aliniambia hataki kusikia taarifa hizo.
“Niliweka msimamo wa kutotoa ujauzito na yeye akasitisha huduma mbalimbali ikiwemo fedha za malipo ya chumba alichonipangia.
“Alianza kunipigia simu na kunitisha kuniachisha kazi aliyonitafutia hotelini bila kupewa malipo yoyote. Alikuwa akinitumia watu mbalimbali kunitishia maisha.
“Kutoka na hali hiyo nililazimika kumtafuta kiongozi mmoja wa ngazi ya juu kanisani na kumwambia jinsi askofu alivyonitelekeza kwa zaidi ya miaka minne bila kunihudumia nikiwa na watoto wake wawili.
“Hata hivyo, kiongozi huyo aliniambia atalishughulikia suala langu, lakini hadi sasa hakuna kinachoendelea na nikimkumbusha amekuwa akinijibu kwa ukali na kunikatia simu.”
WATOTO HAWAENDI SHULE
Peace alisema: “Kwa sasa naishi kwa shida na watoto. Hawaendi shule baada ya kukosa ada.”
ASKOFU ANASEMAJE?
Akizungumza kwa simu na mwandishi wa habari hizi huku akihifadhiwa sauti, Askofu Bagonza alikiri kumtambua Peace kama mzazi mwenzake ila alisema si kweli kama hamtumii matumizi.
“Mbona fedha huwa namtumia labda ameamua kunichafua tu. Hata juzi nimemtumia shilingi 250,000 iweje asema simhudumii?” alisema askofu huyo na kukata simu.
Kwa upande wake, Peace alipoulizwa kuhusu kutumiwa kiasi hicho cha fedha, alisema: “Fedha hizo nilizipokea kutoka kwa wakala wa M-Pesa baada ya jambo hilo kulifikisha kwenye vyombo vya dola (polisi).
”Taarifa zilizolifikia zinaeleza kuwa mwanamke huyo ameitwa Karagwe kwenda kuongelea suala hilo.
0 maoni:
Post a Comment