BURUNDI AMANI YAENDELEA KUTOWEKA, POLISI WAFYATUA RISASI ZA MOTO BAADA YA MAKUNDI YA VIJANA KUANDAMANA WAKIMTAKA RAIS NKURUNZIZA KUTOGOMBEA URAIS.
Makundi ya vijana yaliweka vizuizi barabarani huku wakiimba nyimbo za kumtaka Rais Pierre Nkurunziza abadili msimamo wake wa kutaka kugombea awamu nyingine ya Urais nchini humo.
Maandamano hayo yameanza siku chache baada ya mapinduzi ya kijeshi ambayo hayakufaulu.
Waandishi wa BBC walishuhudia wanajeshi wakifyatua risasi za moto kwa waandamanaji walioonekana wakikimbia kote barabarani.
Biashara kadhaa zilifungwa na shughuli za kawaida kukwama katika maeneo ya Nyakabiga, Musaga na Mutakura.
Hadi kufikia sasa hakuna habari zo zote zilitolewa kuhusiana na waliouawa au kujeruhiwa.
Hata hivyo maeneo anakoungwa mkono Rais na katikati mwa mji shughuli ziliendelea kama kawaida.
Waandamanaji waliambia BBC kuwa wanapinga uamuzi wa Rais Nkurunziza kukugombea awamu ya tatu uongozini.
Jana kiongozi huyo wa Burundi alijitokeza hadharani kwa mara ya kwanza mbele ya vyombo vya habari vya kimataifa lakini hakusema lo lote kuhusiana na hali ya wasiwasi inayokumba taifa lake.
Rais aliyerudi nchini Alhamisi jioni aliwambia waandishi wa habari kuwa Burundi inakabiliwa na vitisho kutoka kwa kundi la magaidi walioko nchini Somalia la Al Shaabab.
Wakati huo huo ubalozi wa Marekani ulitoa taarifa na kuwaomba wafanyakazi wake ambao hawashughulikii maswala ya dharura na familia zao waondoke nchini kwa sababu ya kuendelea kuzorota kwa uchumi.
0 maoni:
Post a Comment