Aliyewahi kuwania jimbo la Arumeru Mashariki kupitia CCM Sioi Sumari akijinadi mbele ya Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha Edward Lowassa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo Mh. Lowassa alikuwa mgeni rasmi(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Mbunge wa Viti Maalum, Namelock Sokoine akinadaiwa na Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha Edward Lowassa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo Mh. Lowassa alikuwa mgeni rasmi
*****
Baadhi ya wagombea waliotangaza nia kuwania ubunge katika majimbo mbalimbali mkoani Arusha kupitia CCM juzi walionekana kupigana vikumbo na wengine wakijinadi mbele ya waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani hapa Edward Lowassa.
Lowasa,ambaye anatajwa kuwania urais kupitia CCM mwaka huu mwishoni mwa wiki iliyopita aliendesha harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi uliopo wilayani Arumeru mkoani Arusha akimwakilisha makanu wa Rais,Dk Mohammed Billal na kufanikiwa kukusanya zaidi ya kiasi cha sh,235 milioni ikiwa ni zaidi ya makisio ya msikiti huo kukusanya sh,200 milioni .
Baadhi ya watia nia wa CCM walionekana wakichangia fedha katika harambee hiyo huku wengine wakitumia mwanya wa kunadi sera pindi walipokaribishwa jukwaa kuu.
Wagombea hao watarajiwa wa ubunge ni Mustapha Panju alitoa Sh6 milioni, Sioi Sumari (Sh7 milioni), Kim Fute (Sh3 milioni), Philemon Mollel (Sh5 milioni), mbunge Peter Serukamba (Sh3 milioni) na mjumbe wa NEC kutoka jimbo la Busega, Dk Raphael Chegeni alichanga Sh1 milioni sawa na mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na Namelock Sokoine.
Hatahivyo,wakati wagombea hao kwa nyakati tofauti mara walipofika kuchangia harambee hiyo na kupewa nafasi ya kusema neno ndipo badhi yao walisikika wakinadi sera kitendo kilichopelekea kuibua shangwe kwa wahudhuriaji.
Mke wa mtia nia wa CCM,Violet Mfuko ambaye mmewe ametangaza nia,Kim Fute alifika jukwaa kuu na kumnadi mmewe kwa kumwambia Lowasa kwamba ametangaza nia na kuwataka makada wa CCM kumuunga mkono.
“Mheshimiwa waziri mkuu mme wangu ametangaza nia jimbo la Arusha mjini,mimi ni mke wake nawaomba jamani mumuunge mkono”alisema Mfuko na kuibua shangwe
Hatahivyo,mtia nia mwingine wa CCM jimbo la Monduli mkoani Arusha,Sokoine naye alipopanda jukwaani Lowasa alitumia nafasi hiyo kumnadi kwa kuwataka makada wa CCM kumuombea kwa Mungu mambo yake yaende vizuri.
“Jamani huyu naye ametangaza nia huko Monduli tumuombee kwa Mungu mambo yake yaende vizuri “alisema Lowasa
Hatahivyo,Sumari,Monaban,Panju na baadhi ya wagombea wengine walipanda jukwaa kuu na kisha kujitambulisha kabla ya kuchangia fedha huku wakitamka ya kwamba wanaomba mambo yao yaende vizuri ili wapitishwe kugombea ndani ya CCM.
0 maoni:
Post a Comment