Jumamosi hii ndiyo mwisho wa Planet bongo-Dullah
Kile kipindi bora kabisaa cha burudani ambacho kilikuwa kikiruka kila siku ya Jumamosi kuanzia saa Nne kamili asubuhi mpka saa sita mchana, Jumamosi hii kinafikia tamati na hakitosikika tena Jumamosi, akipiga stori na Power Jams ya East Africa Radio
wa kipindi hicho Dullah alimaarufu kama Mjukuu amesema kuwa yeye amekua mtangazaji wa kipindi hicho huu mwaka wa saba lakini anasikitika kuachana na kipindi hicho, sababu anatambua kuwa vijana wengi walikuwa wakikifuatilia na kukisikiliza ila hana namna zaidi ya kuwaaga.
"Jumamosi hii Planet Bongo itakuwa ndiyo show ya mwisho kabisaa, Mjukuu wa Ambua ni mwaka wa saba sasa nimekuwa nikiishi nayo hiyo show naamini kabisaa ni stori mbaya hizi sababu mashabiki waliipenda na kila Jumamosi ni show iliyokuwa ikisikilizwa sana asubuhi. Nachoomba mashabiki wangu wasikilize Show ya mwisho wa Planet bongo ili tuagane vizuri hivyo kuna vitu fulani vizuri kama Suprise ambavyo vitakuwepo siku hiyo."
"Mwenyewe nimepokea simu nyingi, Sms na kuona kwenye mitandao ya kijamii watu wakizungumzia suala hilo, ni kweli sitasikika tena katika Planet bogo ya radio baada ya Jumamosi hii, hivyo nawashukuru sana viongozi wa East Africa Radio kwa kuwezesha show hiyo kuwa bora kwa muda wa miaka saba, lakini pia nitioa shukrani za dhati kwa wasanii, marafiki ambao walikuwa na mimi kwa kipindi chote hicho. Aliongeza Dullah.
Mjukuu wa Ambua amesema kuwa kwa wale mashabiki wake sikilize kipindi cha mwisho yeye kufanya ambapo ndipo ataweka wazi baada ya hapo atafanya nini au ataenda wapi baada ya kuweza kutangaza kipindi hicho kwa miaka saba.
0 maoni:
Post a Comment