ANGALIA PICHA UFUNGUZI RASMI WA MAONESHO YA VIWANDA VIDOGO KANDA YA ZIWA YANAYOFANYIKA MJINI SHINYANGA



Hapa ni katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambako panafanyika maonesho ya
 
13 ya Viwanda Vidogo kanda ya ziwa yaliyoandaliwa na Shirika la Viwanda Vidogo 

nchini(SIDO).Pichani kundi la ngoma ya Kisukuma “ Wanunguli” kutoka kijiji cha 

Bugimbagu wilaya ya Shinyanga Vijijini wakitoa burudani,siku ya Jumamosi Mei 

30,2015-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog


Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa  Shinyanga Ally Nassoro Rufunga kwa niaba ya waziri 

wa Viwanda na Biashara nchini Abdallah Kigoda akiwasili katika viwanja vya Shycom 

mjini Shinyanga ambako panafanyika maonesho ya 13 ya Viwanda Vidogo kanda ya 



ziwa yaliyoandaliwa na Shirika la Viwanda Vidogo nchini(SIDO).


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akisalimiana na Viongozi mbalimbali-
Maonesho hayo yamezinduliwa rasmi Mei 30,2015 ingawa maonesho hayo yameanza

Mei 28 mwezi huu na Kilele chake kitakuwa Juni 2015 ambapo wajasiriamali mbalimbali

kutoka ndani na nje ya nchi wanaonesha bidha zao katika Viwanja vya Shycom mjini

Shinyanga.

Katika maonesho hayo jumla ya wajasiriamali 200 kutoka mikoa ya Tanzania bara na

Visiwani pamoja na wajasiriamali kutoka nchini Kenya wanashiriki katika maonesho

 hayo yaliyoandaliwa na uongozi wa SIDO Kanda ya ziwa kwa kushirikiana na ofisi ya

mkuu wa mkoa wa Shinyanga

Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga kwa niaba ya waziri wa

Viwanda na Biashara akikata utepe ishara ya kuzindua rasmi maonesho hayo.Baada ya

kukata utepe mgeni rasmi alitembelea mabanda mbalimbali ya wajasiriamali.Kulia

kwake ni Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Viwanda Vidogo( SIDO) nchini Injinia  Omary
 Bakari
Meneja wwa SIDO mkoa wa Shinyanga Athanas Moshi akitoa maelezo kwa mheni rasmi

kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na SIDO

Kundi la ngoma ya jadi ya Wanunguli wakitoa burudani katika viwanja vya Shycom

 mjini Shinyanga

Wanunguli wakitoa burudani

Meneja wa SIDO mkoa wa Shinyanga Athanas Moshi akizungumza wakati wa Ufunguzi

wa maonesho hayo

Mstahiki  meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo

Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa  Shinyanga Ally Nassoro Rufunga kwa niaba ya waziri

wa Viwanda na Biashara nchini Abdallah Kigoda akitoa hotuba yake ambapo aliwataka

 wajasiriamali nchini kufanya kazi zao kiteknojia zaidi na kuhakikisha wanakuwa

wabunifu zaidi kwa kubaini nini na kipi kinahitajika lini na wapi wakitumia rasilimali

zilizopo katika maeneo yao.



Rufunga alisema ili kuendeleza viwanda nchini wajasiriamali wanatakiwa kuwa

wabunifu zaidi ili kuleta ushindani katika soko la bidhaa wanazozalisha kupitia viwanda

 vyao vidogo.
 
Mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga kwa niaba ya waziri wa

viwanda na biashara alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi wa Shinyanga kutumia

maonesho hayo kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na wajasiriamali kutoka

kanda ya ziwa na wajasiriamali kupata muda wa kubalishana uzoefu wa kazi zao.

Mkuu wa mkoa wa Simiyu Erasto Mbwilo akizungumza wakati wa ufunguzi wa

maonesho hayo

Mjasiriamali Paulina Nyanzala akisoma risala kwa niaba ya wajasiriamali 200 ambapo

 alisema miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo ni pamoja na ukosefu wa 

dhamana zinazohitajika na kukubalika katika taasisi za fedha kwa ajili ya kupata 

mikopo na kwamba changamoto nyingine ni uhaba wa vifungashio vya kisasa 

vinavyokidhi viwango vya ubora na kukabiliana na soko la ushindani.

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Viwanda Vidogo( SIDO) nchini Injinia Omary Bakari

akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo ya Viwanda vidogo Kanda ya ziwa

 ambapo aliwataka wajasiriamali nchini kufanya shughuli zao kiteknolojia na kuwa

wabunifu zaidi ili kuhakikisha kuwa viwanda vidogo vinainua hali ya
o kiuchumi.

0 maoni:

Post a Comment