LEO IMETIMIA MIAKA MIWILI TANGU MWANAMUZIKI ALBERT MANGWEA AAGE DUNIA......R.I.P Ngwair
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete aliwahi kusema anasikitika kuona kwamba zamani watoto walikuwa wakiwazika wazazi wao, lakini katika maisha ya sasa wazazi wamekuwa wakiwazika watoto wao. Ni kweli, na ni jambo la kusikitisha lakini kama wasemavyo, afanyalo Mungu halina makosa

Leo ni miaka miwili tangu rapper Albert Mangwea afariki dunia
kuhusu kifo chake, zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuenea kwa kasi mitaani.
Zilikuwa kama uvumi tu na wengi walihisi ni utani ambao baadaye ungeisha lakini ikaja kubainika kuwa ni habari ya kweli. Ilikuja kufahamika kuwa Ngwair akiwa na rafiki yake M TO THE P waliopelekwa kwenye hospitali ya St Helen ya jijini Johannesburg wakiwa mahututi. Mpaka leo haijulikani kipi kiliwakuta.

Taarifa za kifo cha Ngwair ziliitikisa Tanzania.

tutakutana naye siku ya mwisho na nitamweleza machungu yangu na kwa jinsi gani kifo chake kimeniumiza,” alisema Afande Sele.
Kipaji cha Albert Mangwea katika uandishi wa mashairi ya hip hop na uwezo wa kufanya mitindo huru haukuwa na mfano na bado alikuwa na mustakabali mzuri kimuziki. Ngwair ni miongoni mwa wasanii wa hip hop waliokuwa na hits nyingi na wenye mashabiki wengi.

na YOHANA EMMANUEL
Yohana Blog
0 maoni:
Post a Comment