Hatimaye mgomo wa madereva umemalizika baada ya kufikia makubaliano kati yao na serikali juu ya namna ambavyo madai yao yatakavyoshughulikiwa na serikali.
Awali kabla ya kufikia makubaliano hayo askari
walianza kutoa baadhi ya mabasi chini ya ulinzi mkali wa polisi wa kikosi cha
kutuliza ghasia FFU pamoja na askari wa usalama barabarani zoezi ambalo baada
ya muda lilionekana kukwama kwa kile baadhi ya madereva waliokuwa kituoni hapo
kudai kuwa mgogoro huo hauwezi kumalizika kwa kutumia nguvu.
Harakati za kumaliza mgomo huo zilianza mapema
alfajiri kwa vikao vilivyofanyika kituoni hapo kati ya madereva na wamiliki wa
mabasi na baadae mchana alifika mkuu wa wilaya ya kinondoni ambaye kabla ya
kufikia muafaka huo wakiwa katika mazungumzo vurugu zilizuka gafla ambapo
baadhi ya vijana walianza kurusha mawe kuelekeza kwa viongozi hao wakiwemo
wakuu wa polisi na waandishi wa habari na baadhi ya watu kujeruhiwa hali
iliyowalazimu polisi kutumia mabomu ya machozi.
Mara baada ya kufikia makubaliano hayo katibu wa
chama cha madereva akazungumza na umati wa madereva na abiria waliokuwa kituoni
hapo na kutaja madai .
waliotiliana saini na serikali huku mkuu wa
wilaya ya kinondoni akielezea namna serikali itakavyoshughulikia suala hilo na
yeye atafanya nini endapo halitafanikiwa.
Hata hivyo baada ya mabasi hayo kuanza kutoka
ndani ya kituo hicho baadhi yake yalionekana kutokuwa na abiria ndani
halikadhalika idadi kubwa ya mabasi yakibakia ndani ya kituo hicho.
Kufuatia mgomo huo uliotikisa nchi kutokana na
mamia ya wasafiri kukwama maeneo mbalimbali ya nchi huku abiria wanaotumia
usafiri wa daladala wakilazimika kutembea kwa miguu baadhi ya viongozi wa vyama
vya siasa wamefika kituo kikuu cha mabasi ubungo na kuzungumza na abiria pamoja
na madereva hao akiwemo Mwenyekiti chadema Freeman Mbowe na Prof Ibrahim
Lipumba Mwenyekiti CUF nahivyo shughuli kuanza na dala dala kufanya safari zao
kama kawaida.
0 maoni:
Post a Comment