MWANAMKE ABAKWA NA WANAUME SABA MPAKA KUPOTEZA MAISHA....

MWANAMKE ABAKWA NA WANAUME SABA MPAKA KUPOTEZA MAISHA....

Kuna stori zingine ukizisikia unaweza kufikiri ni utani ama ndoto!!

 Hii  ya leo imetokea mkoani Shinyanga,ambapo
Mwanamke mmoja ambaye anasadikiwa kuwa mkazi wa mtaa wa Matanda katika manispaa ya Shinyanga amefanyiwa vitendo vinavyoelezwa kuwa ni ubakaji na wanaume saba tofauti hali iliyosababisha kupoteza fahamu.

Tukio hilo limetokea leo katika mtaa wa Tambukareli kata ya Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga katika nyumba ya mama aliyefahamika kwa jina la mama Seni ambaye anajihusisha na biashara ya kuuza pombe za kienyeji. 

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema mwanamke huyo ni miongoni mwa wateja wa pombe za kienyeji waliofika kwa mama Seni na baada ya kulewa alianza kuvutwa na wanaume ambao pia ni wateja waliokuwa wamelewa.

Picha;Mwanamke aliyebakwa na wanaume 7 Mkoani Shinyanga

 Wamesema kutokana na hali hiyo ilimlazimu mwenye nyumba ambaye ndiye muuzaji wa pombe za kienyeji kumuingiza mwanamke huyo chumbani pamoja na wanaume waliokuwa wanamvuta ambao ni zaidi ya 7 .

Picha;Nyumbani inayodaiwa kufanyika unyama huo

"Huku kwenye pombe hakuna adabu kabisa,unaambiwa miongoni mwa waliombaka wamo vijana wenye nguvu ,watanashati zaidi ya saba,basi wakamfanyia ukatili ,tunaomba jeshi la polisi litende haki,waliotenda ukatili wapo na wanajulikana kabisa,tunataka wachukuliwa hatua za kisheria",mashuhuda waliongeza.

Picha;Baadhi ya watu wakikamatwa kuhusiana na tukio hilo

Mwenyekiti wa mtaa wa Tambukareli Roja Mshana amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na ametowa wito wa wananchi hasa wanawake kujiepusha na unywaji wa pombe wa kupindukia ili kuzuia vitendo vya ukatili kwa wanawake vinavyoendelea kutokea.

Picha;Baadhi ya watu wakishuhudia

Mwandishi wa habari hizi amefika eneo la tukio na  kushuhudia gari la polisi likiwachukua wanaume watatu wateja wa pombe za kienyeji, muuzaji wa pombe hizo aliyehafamika kwa jina la mama Seni  pamoja na mwanamke aliyefanyiwa vitendo hivyo ambaye inasadikiwa kuwa alikuwa amepoteza fahamu.

0 maoni:

Post a Comment